HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 15, 2021

CRDB Bank Marathon 2021 yafanikiwa kukusanya nusu bilioni kusaidia afya na mazingira

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni 200 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Prof. Mohammed Janabi ambazo zimekusanywa kupitia CRDB Bank Marathon kusaidia upasuaji kwa watoto 100 wenye magonjwa ya moyo. Benki ya CRDB mwaka huu imekusanya Shilingi Milioni 500, ambapo fedha nyengine Shilingi Milioni 104 zimetolewa Taasisi ya Saratani Ocean Road kusaidia ujenzi wa Kituo cha Mawasiliano na fedha zilizobaki zimepelekwa katika kusaidia kampeni kabambe ya mazingira, nchini, Mbio hizi zimefanyika leo katika viwanja vya farasi, Oysterbay, Dar es salaam .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni 104 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt. Julius Mwaiselage ambazo zimekusanywa kupitia CRDB Bank Marathon kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Kituo cha Mawasiliano. Katika mbio hizo za hisani Benki ya CRDB mwaka huu imekusanya Shilingi Milioni 500, ambapo fedha nyengine Shilingi Milioni 200 zimetolewa kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa ajili ya kusaidia gharama za upasuaji kwa watoto wenye magonjwa ya moyo na fedha zilizobaki zimepelekwa katika kusaidia kampeni kabambe ya mazingira  nchini. Mbio hizi zimefanyika leo katika viwanja vya farasi, Oysterbay, Dar es salaam .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya Shilingi Milioni 5 mshindi wa kwanza wa mbio za 42km kwa upande wanawake katika CRDB Bank Marathon, Shelmith Nyawira raia wa Kenya. Katika mbio hizo Benki ya CRDB imekusanya jumla ya Shilingi Milioni 500 kwa ajili ya kusaidia watoto wenye upasuaji wa moyo JKCI, kujenga Kituo cha Mawasiliano Taasisi ya Saratani Ocean Road na kampeni kabambe ya mazingira nchini, Mbio hizi zimefanyika leo katika viwanja vya farasi, Oysterbay, Dar es salaam .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya Shilingi Milioni 5 mshindi wa kwanza wa mbio za 42km kwa upande wa wanaume katika CRDB Bank Marathon, Paulo Ayanaye raia wa Kenya. Katika mbio hizo Benki ya CRDB imekusanya jumla ya Shilingi Milioni 500 kwa ajili ya kusaidia watoto wenye upasuaji wa moyo JKCI, kujenga Kituo cha Mawasiliano Taasisi ya Saratani Ocean Road na kampeni kabambe ya mazingira nchini, Mbio hizi zimefanyika leo katika viwanja vya farasi, Oysterbay, Dar es salaam . 
Mbio za hisani zakimataifa zilizoandaliwa na Benki ya CRDB “CRDB Bank International Marathon” kwa mwaka 2021 zimefanikiwakuandika rekodi kwa kuvutia washiriki zaidi ya 5,000 ikiwamo maelfu ya raia wa kigeni. Jumla ya Shilingi zaKitazania Shilingi milioni 500 zimefanikiwa kukusanywaambazo zitaelekezwa kwa ajili ya kusaidia jamii.

Akizungumza na washiriki, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mbiohizo, aliipongeza Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti naWafanyakazi wote wa Benki ya CRDB kwa kufanikishambio hizo zilizokuwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajiliya watoto wenye uhitaji wa upasuaji wa moyo JKCI, kujenga kituo cha mawasiliano cha Taasisi ya Saratani yaOcean Road (ORCI) na kusaidia utunzaji mazingira kupitiakampeni ya Pendezesha Tanzania.

Waziri Majaliwa alisema kuwa Serikali inasikia faharikuona taasisi za kizalendo kama Benki ya CRDB zikiwamstari wa mbele katika kusaidia Serikali kuboresha sekta zakijamii kama vile; afya, elimu na mazingira na huku akikirikwa dhati kuwa mbizo hizo zinazofanyika kila mwakakuwa ni fursa adhimu ya kuchangisha fedha kwa ajili yakuwekeza katika ustawi wa jamii.

“Nimekuja hapa kwa lengo la kuonyesha kuwa Serikaliinaunga mkono na kufurahishwa sana na ubunifu huu waBenki ya CRDB. Kwa niaba ya Serikali niwashukuru kwakushirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) kwakuboresha huduma za afya kwa umma,” anaeleza Waziri Mkuu.

Aliwapa kongole viongozi mbalimbali wa Serikaliikiwamo; Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, Naibu Waziri mwenye dhamana ya Michezo, Pauline Gekul, NaibuWaziri wa Afya, Dk Godwin Mollel na washiriki wenginewote kwa kuunga mkono jitihada hizo ambazozimejielekeza katika kuokoa maisha ya wale wenye uhitajikatika jamii na kuboresha mazingira.

“Nafahamu wazi kuwa ni ngumu miongoni mwenu kuamkaasubuhi sana hususan katika hali hii ya hewa ya baridi nasiku za mapumziko, lakini mmeweza kuzishinda nafsi zenuna kuacha shuka zenu pembeni ili kuja kushiriki katikambio hizi,” aliongezea.

Alipongeza uamuzi wa Benki ya CRDB kuendelea kusaidiaupasuaji wa watoto wenye magonjwa ya moyo. Waziri Mkuu alisema uamuzi huo utaendelea kusaidia kupunguzamakali ya gharama kwa ajili ya upasuaji wa moyo ambazowatu wengi hawawezi kuzimudu  pamoja na Serikali kutoaruzuku ya asilimia 80.

“Wazo hili la kuendelea kusaidia gharama za upasuaji kwawatoto ni uamuzi mzuri sana kwani hata asilimia 20 iliyobaki wazazi wengi hawana uwezo wa kuchangia. Hongereni kwa kurejesha tabasamu kwa watoto nakuwapatia tumaini la maisha,” Waziri Majaliwa alisisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alibainisha kuwa mbizo za mwaka huuzimevuka lengo la ukusanyaji wa Shilingi milioni 500, akitoa shukrani kwa makampuni na taasisi zilizojitokezakushirikiana na benki hiyo pamoja na wakimbiajiwaliojitokeza kutoka ndani na nje ya nchi.

“Kati ya fedha zote Shilingi Milioni 500 zilizopatikanakatika mbio hizo, Shilingi Milioni 200 zimeelekezwa JKCI, Sh104 milioni zimeenda ORCI na kiasi kilichobakikimeelekezwa katika kampeni za utunzaji wa mazingira,” alisema Nsekela.

Nsekela aliwashukuru Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof, Mohammed Janabi na Mkurugenzi Mkuu wa ORCI, Dkt.Julius Mwaiselage kwa ushirikiano wao huku akiwekamkazo kuwa kauli mbiu ya benki hiyo isemayo “Kasi Isambazayo Tabasamu” imefanikiwa kutokana na mchangowao wa dhati.

Katika maelezo yake ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Mkurugenzi wa MawasilianoBenki ya CRDB, Tully Mwambapa alisema asilimia 85 yawashiriki wa mbio hizo ni Watanzania huku akibainishakuwa wakimbiaji wa kimataifa waliojisali kutoka nje yaTanzania ni zaidi ya 700.

Akiongezea, Tully alisema mbio hizo za CRDB Bank International Marathon ambazo zimeendelea kutambulikakimataifa baada ya kupatiwa ithibati na World Athletics naAMIS, kwa sasa zina hadhi sawa na zile mbio za Sanlam Cape Town Marathon za Afrika Kusini na Boston Marathon za nchini Marekani.

“Ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa mbio hizi za CRDB zinarejesha heshima ya Tanzania ya michezo katika taswiraya dunia,” anaeleza Tully. Huku zaidi ya wakimbiaji wakimataifa 700 wakishiriki katika mbio za mwaka huu.

Mbio hizo zimeendelea kupata mwamko mkubwa kutokakwa wakimbiaji kutokana na lengo lake la kusaidia kusaidiajamii. Hii ni mara ya pili Benki ya CRDB inaandaa mbiohizi kwa mafanikio makubwa, baada ya zile zilizofanyikamwaka na kukusanya Shilingi Milioni 200 kwa ajili yaupasuaji wa watoto katika Taasisi ya Moyo ya JakayaKikwete. Mbio za mwaka jana zilizinduliwa na Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhuambaye kwa wakati huo alikuwa akihudumu kama Makamuwa Rais.

Katika matokeo ya mbio hizo, Paulo Ayanaye raia waKenya aliibuka kinara wa mbio za 42km kwa upande wawanaume akitumi muda wa 02:15:28, wakati ShelmithNyawira raia wa Tanzania aliibuka mshindi kwa upande wawanawake akitumia muda wa. Kwa mbio za 21km, mshindikwa upande wa wanaume alikuwa Mkungo Panuel raia waKenya akitumia muda wa 01:03:19, kwa upande wawanawake mshindi alikuwa Pauline Esikon raia wa Kenya baada ya kutumia muda wa 01:12:17.

Katika10km, mshindi kwa upande wa wanaume alikuwaJoseph Tiophil raia wa Tanzania alitumia muda wa00:28:51, kwa wanawake Transfora Musa raia wa Tanzania ameshika nafasi ya kwanza baada ya kutumia muda wa00:33:52.

Katika mashindano ya mbio za baiskeli 65km, MasungaDuba raia wa Tanzania aliibuka mshindi kwa upande wawanaume baada ya kutumia muda wa 01:49:07, upande wawanawake Swabra Abdallah raia wa Tanzania ameibukamshindi baada ya kutumia muda wa 02:06:39. Washindi 32 katika mbio hizo wamejizolea jumla ya Shilingi Milioni 50.













No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad