HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 8, 2021

WATUMISHI HOSING (WHC) SHIRIKISHAANENI NA TAASISI ZINGINE ZA UMMA- MUHAGAMA

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu) Jenista Muhagama ameliagiza Shirika la Nyumba la Watumishi Hosing  (WHC) kushirikisha Taasisi  zingine za umma zinazotoa huduma muhimu kwa Jamii  ili kupunguza gharama za maisha kwa wapangaji.
Waziri Jenister alitoa agizo hilo Dar es Salaam,jana  baada ya kutembelea mradi  wa nyumba 65 za Shirika hilo zilizojengwa maeneo ya  Bunju B na kubaini changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa barabara na shule.
Alisema mradi mkubwa kukosa huduma muhimu  sio jambo zuri kwani  inawapa changamoto wahitaji  kwenda  kutafuta huduma hizo mbali badala ya kuendelea kufanya shughuli  zao za kiuchumi.
“Naagiza  kwa viongozi wa watumishi housing katika  miradi mingine mikubwa  inayokuja lazima tushirikishe  na mamlaka zingine za kutoa huduma muhimu kama maji barabara na huduma zingine  kama zahanati  na shule ziwe karibu kwa sababu uhitaji unakuwa makubwa",alisema Jenista
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kutembelea Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Bunju B wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)
Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa (kushoto) akizungumza aki akitoa maelekezo kuhusu mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Bunju B wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Jenista Mhagama, (katikati) akiwa ameambatana na watendani mbalimbali  wakitembelea Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Bunju B wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa majengo ya Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Bunju B wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad