Na WAMJW - Moshi, Kilimanjaro.
Wanachama
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wametakiwa kuhakikisha
wanatumia kadi za uanachama wao katika kufanya malipo halali ya huduma
wanazopata katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Rai
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel alipokuwa
ziara katika Mkoa wa Kilimanjaro na kupokea ripoti ya ubadhirifu wa NHIF
unaofanywa na wanachama pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya.
"Kila
Mtanzania ahakikishe kadi yake ya bima ya afya inatumika kufanya malipo
halali tuu, kila mwenye duka la dawa ahakikishe anaposaini fomu za bima
ya afya na anapopokea na kudai madai, adai malipo halali tuu" amesema
Dkt. Mollel
Dkt. Mollel
amezitaka taasisi za umma na binafsi zinazotoa huduma za afya nchini
kuhakikisha kadi za bima ya afya zinatumika kwenye malipo halali huku
wakiwasimamia vyema watumishi hao wasijiingize katika vitendo vya wizi
kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Amesema
kuwa wanachama pamoja na watumishi watakaobainika kujihusisha na
vitendo hivyo vya wizi kwa mfuko watatakiwa kurejesha fedha zote
walizosababishia hasara NHIF pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria
chini ya vyombo vya dola.
Dkt.
Mollel amesema kuwa tusipokuwa matumizi mazuri na kuwa na uadilifu
ndani ya mfuko wa bima ya afya huku ubadhirifu ukiendelea, adhma ya Rais
wetu Mama Samia Suluhu Hassan ya kuwa na mfuko imara wa bima ya afya
kwa wote hapa nchibi hatutoifikia.
"Rais
wetu Mama Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya Shilingi Bilioni 148 kwa
ajili ya mfuko wa bima ya afya kwenda kuwasaidia wananchi wasiokuwa na
uwezo kuwa na uhakika wa bima, sisi tunaosimamia mifumo, tusiposimamia
kuondoa uchafu na ubadhirifu wote mfuko huu utakufa" amefafanua Dkt.
Godwin Mollel.
Aidha
Dkt. Mollel amesema kuwa wataenda kuchunguza pia watumishi wa afya
katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF na endapo watabainika
kujihusisha na vitendo hivyo vya ubadhirifu hatua kali za kisheria
zitatumika dhidi yao.
Awali
akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Stephen Kigaigai amesema
kuwa uchunguzi uliofanywa na NHIF pamoja na vyombo vya usalama umebaini
ubadhirifu wa shilingi milioni 520 uliosababishwa na vituo 12 vya
kutolea huduma za afya, watumishi wa aya kutoka hospitali 38 na
wanachama 6 wa mfuko huo.
"Ubadhirifu
huu haukubaliki, natoa maelekezo kwa vyombo vya usalama wachukue hatua
za haraka sana kuhakikisha kwamba fedha hizo zinarejeshwa na kuchukuliwa
hatua za kisheria" amesema Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Stephen
Kagaigai.
No comments:
Post a Comment