HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 27, 2021

RAIS DK. MWINYI AWATAKA WADAU KUJITOKEZA KUUNGA MKONO UJENZI WA MABWENI YA WANAFUNZI KAMPASI YA KARUME-ZANZIBAR

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla akizungumza katika hafla ya  uwekaji wa Jiwe la msingi la Ujenzi wa Mabweni ya Chuo cha Kumbukuku cha  Mwalimu Nyerere  Kampas ya Zanzibar.Baadhi ya washiriki katika uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi la Chuo cha Kumbukukumbu  cha Mwalimu Nyerere Kampas ya Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla akiweka Jiwe la msingi la Ujenzi wa Mabweni ya Chuo cha Kumbukuku cha  Mwalimu Nyerere  Kampas ya Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema uwepo wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu  Nyerere visiwani Zanzibar  ni kielelezo Chanya katika kuenzi na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa Vitendo.

Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameleza hayo kupitia hotuba alioisoma kwa niaba ya Rais Dk. Hussein Mwinyi  katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi  wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere – Kampasi ya Karume Zanzibar.

Ameleza kuwa, Bodi pamoja na uongozi wa chuo hicho wamekuwa wakifanya kazi nzuri kwani tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mnamo mwaka 1961 mpaka sasa chuo kimekuwa kinaishi kwa mawazo ya waasisi wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu J.K Nyerere na Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.

Alifafanua kuwa, Ni ukweli usiopingika wahitimu wanaotoka katika chuo hicho baada ya kumaliza mafunzo yao hutoka wakiwa wameiva , wenye uwadilifu na uweledi wa hali ya juu jambo ambalo lina umuhimu kwa watu ambao hupewa dhamana katika nafasi za utumishi wa Umma.

Pamoja na mambo mengine, Makamu wa Pili wa Rais amemuomba mkandarasi wa mradi huo ambae ni SUMA JKT kukamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa kwani mradi huo unalenga kutatua changamoto kubwa iliopo kwa wanafunzi ya kukosa makaazi.

Kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Mohamed Said ameupongeza uongozi wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuhakikisha yale malengo waliojiwekea ya kutoa mafunzo ya uongozi na uzalendo kwa jamii yanafikiwa.

Aidha, Mhe. Simai aliukumbusha uongozi wa Chuo hicho mbali na mafunzo ya uongozi na uzalendo wanayoyatoa lakini pia ipo haya yua kuangalia upya uwezekano wa kuwafanya wanafunzi wawe na uwezo wa kufanya vitu vingi kwa pamoja kwa kuzingatia masuala ya Ubunifu na Uvumbuzi kama zinavyofanya nchi nyengine Duniani.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila ametumia fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa jitihada anazoendelea katika kukuza uchumi wa Zanzibar.

Akigusia changamoto zinazokikabili chuo hicho kwa kampasi ya Karume Zanzibar amesema kumekuwepo kwa changamoto ya baadhi ya watu kuvamia eneo la chuo tangu mwaka 2018 na kumuomba mgeni rasmi kulipatia ufumbuzi suala hilo kutokana na kurejesha nyuma jitihada za chuo hicho.

Akisoma Taarifa ya utekelezaji wa mradi huo  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la uzalishaji Mali la jeshi la kujenga Taifa (SUMA-JKT) Kanali Absolonon Lyanga Shausi amesema wanaishukuru serikali ya mapinduzi Zanzibar kupitia wakala wa majengo Zanzibar kwa kuisajili SUMA-JKT kuweza kufanya kazi zake Zanzibar na kuahidi kuwa mradi huo utakamilika ndani ya wakati uliopangwa wa kipindi cha miezi 18 huku ikizingatia weledi katika utekelezaji wake. 

Katika kuunga mkono jitihada za kukamilisha mradi wa ujenzi huo Mbunge wa Jimbo la Mpendae kwa niaba ya Turky Foundation amechangia jumla ya Shiliingi Millioni Ishirini (20,000,000/=) ikiwa ni kuitikia wito wa wadau wa maendeleo waliopo Zanzibar kujitokeza kusaidia kufanikisha mradi huo. 

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

Julai 26, 2021.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad