HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 23, 2021

NMB Yakabidhi Madawati ya Sh. Milioni 10/- Mkuranga

 

  Benki ya NMB imetoa msaada wa viti 50, meza 50 kwa shule ya Sekondari ya Mkugilo na madawati 62 kwa Shule ya Msingi Chatembo, wilayani Mkuranga, Pwani vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 10.

 Msaada huo, ulitolewa katika hafla iliyofanyika viwanja vya Shule ya Sekondari Mkugilo na Meneja Mahusiano, Biashara za Serikali wa NMB Kanda ya Mashabiki, Aneth Kwayu kwa niaba ya NMB na kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Khadija Nasser Ally.

 Akizungumza katika hafla hiyo Aneth alisema kuwa NMB inazitazama changamoto za Sekta ya Elimu kama moja ya vipaumbele vyake vikuu, kutokana na ukweli kuwa elimu ndio ufunguo wa maendeleo sio tu ya mtu mmoja mmoja, bali pia kwa Taifa kwa ujumla- hivyo walivyopata maombi kuzisaidia shule hizi mbili waliona uhitaji na wamezisaidia.

 NMB inatambua jitihada za Serikali katika kuboresha Elimu nchini na kama wadau wameahidi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo za kusaidia jamii, ambayo wanamini ndiyo imeifanya NMB kuendea kuwa benki bora nchini.

 “Tunawashukuru viongozi wa shule mbalimbali nchini wanavyoichagua NMB wanapokuwa na uhitaji, hii inaonesha kuwa mnathamini mchango wetu kwa maendeleo ya jamii. Na sisi tunafurahia kujitoa kwetu na tutahakikishia jamii inayotuzunguka inanufaika na faida tuipatayo," alisema Kwayu.

 Akizungumza wakati akipokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Khadija Nasser Ally aliimwagia sifa NMB kwa namna ilivyojipambanua katika usaidizi na utatuzi wa changamoto za Sekta ya Elimu na Afya nchini, na kwamba yeye sio tu balozi mwema, bali pia ni shuhuda wa harakati chanya za benki hiyo katika kunyanyua elimu kote nchini.

 Msaada huu, ni sehemu ya NMB kutatua changamoto zinazozikabili Sekta ya Elimu nchini lakini pia ni sehemu ya kurudisha kwa jamii sehemu ya faida baada ya kodi wanayoipata kila mwaka.

 

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Khadija Nassir Ally (katikati) akiangalia Viti na Meza 50 baada ya kukabidhiwa na Benki ya NMB kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mkugilo pamoja na madawati 62 kwa ajili ya Shule ya Msingi, Chatembo iliyopo Mwandege wakati wa hafla ya makabidhiano .Kushoto ni  Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mkuranga, Peter Msaki na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mkuranga, Mshamu Munde.

 

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Khadija Nassir Ally, akionyeshwa Meza na Viti na Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mkuranga, Peter Msaki vilivyolewa na Benki ya NMB kwa Shule ya Sekondari Mkugilo pamoja na madawati 62 kwa Shule ya Msingi, Chatembo iliyopo Mwandege  vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 10. Kulia ni Meneja Mahusiano wa Benki ya NMB wa Biashara za Serikali, Aneth Kwayu.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad