HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 21, 2021

Mradi wa kuimarisha Mifumo ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wazinduliwa Zanzibar

 

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Khamis Juma amesema serikali inathamini michango ya wanasayansi katika uibuaji wa tafiti mbalimbali zenye lengo la kuondoa changamoto zinazokabili taifa.

Alisema hayo jana wakati akizindua mradi wa kuimarisha mifumo ya sayansi, teknolojia na ubunifu nchini Tanzania wenye lengo la kwenda sanjari na maendeleo endelevu ya dunia.

Mradi huo unafanyika chini ya ushirikiano wa UNESCO, Tume ya Taifa ya UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.

Alisema kutokana na umuhimu wa mradi huo serikali imewataka wadau wote kutoa ushirikiano wa kutosha kuweka misingi ya utafiti, uendelevu wake na kusaidia watunga sera kutambua nguvu kubwa ya taifa katika kusaidia kubadili maisha ya wananchi kupitia tafiti.

Katibu Mkuu huyo akifafanua zaidi alisema kwamba ni matumaini ya serikali washiriki watasaidia kuchangia uandishi wa msingi wa ripoti itakayowezesha uimarishaji wa hatua za kuimarisha sera na ubunifu katika sayansi na teknolojia.

Aliwataka wadau kuunga mkono jitihada za serikali na UNESCO za kuimarisha utafiti wa kisayansi na ubunifu ili  kuchangia kiuchumi na kujikinga na majanga

Mkuu wa Ofisi, UNESCO Dar es Salaam, Dos Santos Tirso katika hotuba yake ilyosomwa na Mkuu wa kitengo cha Elimu UNESCO, Bi. Faith Shayo alisema kwamba shirika hilo limefurahishwa kufanyakazi na serikali kuhakikisha mradi huo unafanikiwa.

Alisema mradi huo umelenga kusaidia Mataifa Wanachama kutekeleza Pendekezo la Watafiti wa Sayansi na Teknolojia 2017, kwa nchi sita za Afrika tangu Septemba 2020 za Ghana & Sierra Leone,Tanzania, Namibia, Zimbambwe na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mradi utatekelezwa kwa awamu mbili na awamu ya majaribio ya: Septemba 2020 -Agosti 2022 na Awamu ya II: Septemba 2022- Agosti 2025. Bajeti iliyotengwa kwa awamu ya majaribio ya mradi nchini Tanzania ni Dola za Marekani 250,000.

Awali akitambulisha mradi huo Mkuu wa kitengo cha Sayansi asilia na Mratibu wa mradi huo kutoka UNESCO, Bw. Keven Robert alisema kuwa mradi huo utawezesha kusaidia nchi kuimarisha mifumo ya sayansi, teknolojia na utafiti.

 Aidha mradi huo pia utasaidia kuimarisha taasisi za kisayansi kufanya tafiti na kuweka mazingira wezeshi ya kufanya tafiti za kisayansi ambazo zitasaidia katika kutatua changamoto za wananchi, kukabiliana na majanga yakiwemo magonjwa mbalimbali na pia kufikia malengo ya maendeleo endelevu.

 Robert alisema kuwa mradi huo utakuwa na maeneo10 ya utekelezaji ambapo baadhi ya maeneo ni pamoja na kuangalia uwekezaji katika tafiti za kisayansi ambapo matokeo ya tafiti hizo zinapouzwa zinaweza kuimarisha uchumi ya nchi.

“Mfano katika kipindi hiki cha janga la Corona yapo mataifa yaliyofanya tafiti za kisayansi na kutengeneza chanjo hivyo zinapouzwa mataifa hayo yamekuwa yakipata fedha na kukua kiuchumi,” alisema Robert.

Alitaja maeneo mengine yatakayoangaliwa katika mradi huo kuwa ni kwa namna gani tafiti za kisanyansi zinasaidia wananchi na kwa namna gani wananchi wanashirikishwa kwenye tafiti kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali visiwani Zanzibar, Bw. Ali Khamis Juma (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuboresha mifumo ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya UNESCO katika hafla fupi iliyofanyika kwenye hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar. Kulia ni Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel na kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO, Bi Faith Shayo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO, Bi Faith Shayo akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuboresha mifumo ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya UNESCO katika hafla fupi iliyofanyika kwenye hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar.
Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel akitoa salamu za NATCOM wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuboresha mifumo ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya UNESCO katika hafla fupi iliyofanyika kwenye hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar.
Mkuu wa kitengo cha Sayansi asilia na Mratibu wa mradi huo kutoka UNESCO Keven Robert akitoa muhtasari wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu (STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania bara na visiwani kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya UNESCO katika hafla fupi iliyofanyika kwenye hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar.
Meza kuu kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO, Bi Faith Shayo, Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali visiwani Zanzibar, Bw. Ali Khamis Juma pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu (STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania bara na visiwani kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya UNESCO katika hafla fupi iliyofanyika kwenye hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali visiwani Zanzibar, Bw. Ali Khamis Juma (katikati) akikata utepe kama ishara ya kuzindua mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania bara na visiwani kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia bara na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar Wanashiriki tukio hilo ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha Elimu wa shirika hilo nchini, Bi.Faith Shayo (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel (kulia).
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali visiwani Zanzibar, Bw. Ali Khamis Juma (wa tatu kulia) akimkabidhi Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri Elekezi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), Dr Ali Ussi nakala ya mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania bara na visiwani kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia bara na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha Elimu wa shirika hilo nchini, Bi.Faith Shayo (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel (kulia).
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali visiwani Zanzibar, Bw. Ali Khamis Juma (wa tatu kulia) akimkabidhi Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Yahya Abdulla nakala ya mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania bara na visiwani kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia bara na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha Elimu wa shirika hilo nchini, Bi.Faith Shayo (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel (kulia).
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali visiwani Zanzibar, Bw. Ali Khamis Juma (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Elimu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bw. Omar Ali nakala ya mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania bara na visiwani kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia bara na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha Elimu wa shirika hilo nchini, Bi.Faith Shayo (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel (kulia).
Baadhi ya washiriki kutoka taasisi mbalimbali za sekta binafsi, serikali, waandishi wa habari pamoja na jamii walioshiriki uzinduzi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania bara na visiwani unaoratibiwa na UNESCO  kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia bara na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar.
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad