HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 8, 2021

Dkt.Ndugulile ahimiza wananchi wahakiki namba zao za laini za simu

 *Wakati ukifika laini hizo zitafungwa

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile amesema kuwa wananchi wahakiki laini zao za simu kwa usalama wao katika matumizi ya mawasiliano.

Dk.Ndugulile ameyasema hayo wakati alipotembelea Banda la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea kufanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam, amesema kuwa laini hizo wakati ukifika zitafungwa hawawezi kutumia laini hizo pamoja na simu kinachofuata ni kwenda Mamlaka Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Dk.Ndugulile amesema wananchi wahakiki laini zao kutokana na muda ulioopo itafika wakati hawataweza kutumia laini hizo pamoja na simu.

Amesema kuwa uhakiki wa namba ni kumtambua mmiliki wa namba na pale anapobaini kuna namba zingine ambazo sio zake basi anatakiwa kutoa kwa kwenda kwa mtoa huduma wa simu za mkononi kutokana na laini anayoitumia.

Katika maonesho hayo Dkt.Ndugulile aliwataka wananchi kutumia fursa ya maonesho kupata taarifa katika mamlaka ya Udhibiti TCRA.

Aidha Dk.Ndugulile amesema kuwa kuendelea kutumia laini ambayo hajakikiwa kwani kuna wakati mwingine baadhi ya watu walisajiliwa kwa kwa kitambulisho cha mtu mwingine hivyo chochote kikitokea atahusika mwenye jina katika kitambulisho.

"Nitoe rai wananchi wahakiki namba zao za simu kwa usalama wao katika matumizi ya mawasiliano kwa kuweza kujiepusha madhara watayoyapata kutokana na kutosajili namba zao."Amesema Dkt.Ndugulile.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile akizungumza kuhusiana na uhakiki wa laini za simu za mkononi wakati alipotembelea Banda la TCRA maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari Katika Banda la TCRA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea kufanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  Dk.Faustine Ndugulile akikabidhiwa mfuko  wenye machapisho mbalimbali kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Lucy Mbogoro wakati Waziri huyo alipotembelea Banda la TCRA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea kufanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile akisaini kitabu wakati alipotembelea Banda la TCRA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea kufanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

1 comment:

  1. Awesome and interesting article. Great things you've always shared with us. Thanks. Just continue composing this type of post.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad