HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 14, 2021

BRELA YANG’ARA MAONESHO YA SABASABA

 


Picha za ushindi za wafanyakazi wa BRELA  wakati wa Kilele cha maonesho ya Sabasaba.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA) Godfrey Nyaisi  wa akipokea kombe la Mshindi wa Tatu kwa Kundi la Usajili  kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.Suleiman Hemed Abdulla wakati wa kufunga Maonesho ya 45 ya Biashara Sabasaba jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wakiwa na cheti cha ushindi wakati ufungaji wa Maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yaliyomalizika Julai 13 mwaka huu.

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeng’ara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yaliyofikia tamati leo Julai 13, 2021 katika Uwanja wa Mwalimu J.K Nyerere, Dar es Salaam.

Katika maonesho hayo BRELA imeibuka mshindi wa tatu katika kundi la Washiriki wa maonesho hayo wanaojihusisha na Uwezeshaji biashara na Uwekezaji.

Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa washindi wa tatu Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa amebainisha kwamba ushindi huo ni chachu kwa ajili ya kuboresha huduma na kuwafikia watanzania wengi zaidi.

“Kwa sasa tunajiandaa na mpango wa kuwafikia wadau wetu waliopo katika Mikoa 16, huu ukiwa ni mwendelezo wa zoezi la kuwafikia wateja wetu popote pale walipo," alifafanua Bw. Nyaisa.

Alisema pia kuwa  BRELA imekwishatoa elimu katika mikoa ya Njombe Singida, Ruvuma, Dodoma, Iringa na Morogoro, lengo likiwa  ni kuwafikia wadau  katika maeneo yao na kuwahamasisha kuhusu urasimishaji wa biashara na kufanya usajili wa papo kwa papo.

Tangu kuanza kwa maonesho hayo Juni 28, 2021 BRELA imekuwa ikikutana na wadau wake na kuwatatulia changamoto zao papo kwa hapo na kutoa elimu kuhusu huduma zake ili kuwahamasisha Wadau mbalimbali  kurasimisha biashara zao.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano BRELA, Bi. Roida Andusamile ameeleza kwamba katika siku 16 za maonesho hayo zaidi ya watu elfu moja walifika katika banda na kupatiwa Elimu za papo kwa papo.

“Wadau waliojiandikisha kufika katika mabanda yetu ni 1200 na kati ya hao 618  walipatiwa huduma za papo kwa papo za  usajili wa majina ya biashara, usajili wa makapuni, leseni za biashara kundi A na alama za biashara, pia  wengine walipata elimu kuhusu huduma zetu na ushauri pia.” alisema Bi. Andusamile.

Maonesho hayo yalizinduliwa rasmi Julai 5, 2021 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na kufungwa na Makamu wa pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad