HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 29, 2021

WAZIRI MCHENGERWA AWAAGIZA WATUMISHI HOUSING KUJENGA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU KATIKA MAJIJI,MIKOA


Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa (kushoto) akizungumza jambo na Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mohammed Mchengelwa wakati wa ziara ya kutembelea mradi ya ujenzi wa nyumba wa Gezaulole wilaya ya  Kigamboni Mkoa wa  Dar es Salaam.(Picha zote na Emmanuel Mssaka wa Michuzi Tv)
Mkurugenzi wa Uendeshaji na Miradi,Sephania Solomon kanyoosha mikono aki akitoa maelekezo kuhusu mradi nyumba wa Gezaulole, Wilaya ya  Kigamboni  mkoa wa Dar es Salaam  Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mohammed Mchengelwa wapili (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Fatuma NyangasaWaziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mohammed Mchengelwa (katikati) akiwa ameambatana na  na ziongozi wa Wilaya ya Kigamboni na  watendani mbalimbali  wakitembelea Miradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Gezaulole wilaya ya Kigamboni Mkoa wa  Dar es Salaam.

Muonekano wa Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Gezaulole wilaya ya Kigamboni Mkoa wa  Dar es Salaam.
Watumishi wakimsikiliza Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mohammed Mchengelwa.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)



Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

WATUMISHI Housing Company imeagizwa kujenga nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya watumishi katika majiji, mikoa na maeneo yasiyofikika kirahisi ili kuhakikisha watumishi 

Aidha WHC imeagizwa kuandaa mikakati ya kuangalia namna ya kumaliza upungufu wa nyumba za walimu hasa maeneo ya vijijini ili wanapopangiwa vituo vyao vya kazi wasikimbie.Maagizo hayo yanakuka siku mbili tu baada ya Serikali kuwapandisha madaraja watumishi zaidi ya 116,000.

Maagizo hayo yametolewa leo Juni 28,2021 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora Mohammed Omar Mchengerwa ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alipotembelea WHC.

Ametumia nafasi hiyo kuzungumza na wafanyakazi wa watumishi wa WHC ambapo amewataka kufanya kazi kwa weledi na kujituma huku akiwaambia kuwa Serikali imedhamiria kurudisha hadhi ya watumishi wa Umma.

Akizungumza zaidi, amesema hadi jana watumishi 116,000 walikuwa wamepandishwa madaraja ambapo baadhi yao ambao majina yaliwahi wataanza kuona mabadiliko ya kiwango cha mshahara mwezi huu na wale waliochelewa wataanza kuona mwezi ujao kadri tunavyokwenda,”

“Sh.bilioni 300 zilitengewa ajili ya nyingeza za mishahara kwa watumishi ambao wamepandishwa madaraja.Ofisi yangu kwa sababu idadi ya namba inaongezeka  tumemuomba aridhie kuongeza idadi hivyo huenda kwa mwezi ujao tupandishe madaraja watumishi wengine kwa sababu zipo taasisi ambazo zilichelewa kuleta majina ya watumishi,”

"Kwa ofisi zilizochelewa kuleta majina  hatua zitachukuliwa kwa Wakurugenzi wote huku maofisa utumishi wa ofisi hizo wataondoshwa katika nafasi zao kwani wanawanyima fursa watumishi ya kupandishwa madaraja ambayo ni haki yao,"amesema.

Akizungumzia nyumba za watumishi Waziri Mchengerwa amesema lengo lao ni kuhakikisha kero ya makazi kwa watumishi wa umma inatatuliwa hasa maeneo yaliyo na watumishi wengi wa umma kwani kupanga nyumba binafsi kunawaongeza mzigo wa gharama za maisha

Amewaomba watendaji wa WHC wajipange na  kuangalia ni namna gani wanaweza kumaliza kero za watumishi wa umma hapa nchini, hivyo watengeneze mipango na wawe wabunifu ili wamalize hilo.

Ameongeza kwa  watumishi wa kawaida ni ngumu kwao kukusanya hadi Sh.milioni 100 kwa ajili ya kununua nyumba huku akilitaka shirika hilo kutokujiweka kibiashara kwani watakuwa wametoka katika msingi wa kuanzishwa kwa shirika hilo ambalo ni kusaidia watumishi

Kuhusu walimu ambao ni karibu asilimia 60 hadi 70 ya watumishi wa umma nchini kwa mujibu wake aliitaka WHC waangalie namna ya kumaliza kero ya nyumba za walimu hasa katika maeneo ambayo hayafikiki kirahisi.

“Yapo maeneo ambayo tunawapeleka walimu wanashindwa  kukaa kwa sababu hakuna nyumba, yapo maeneo ambayo ni mbali sana hakuna nyumba zenye hadhi ya walimu, hivyo eneo hili pia mlifanyie ubunifu ili muweze kumaliza kero ya nyumba za walimu kote nchini,”

“Lakini hili ni kwa kuzingatia zaidi maeneo ambayo hayafikiki kirahisi ili tunapowapeleka wasikimbie maeneo yao ya kazi,” alisema Mchengerwa

Katika hatua nyingine waziri alisema leo mfumo maalumu wa upokeaji kero uitwao E-mrejesho sema na waziri wa utumishi utazinduliwa jijini Dodoma utakaorahisisha utatuaji kero za watumishi wa umma kutoka maeneo yote nchini

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WHC, Dk.Fred Msemwa aliahidi kufanyia kazi maelekezo yote aliyopewa huku akitaja changamoto zinazowakabili ambapo miongoni mwake ni mtaji mdogo, uhaba wa viwanja katika majiji.

“Pia tunakabiliwa na uhaba wa miundombinu kama maji, umeme na barabara, upatikanaji wa mikopo nafuu na muda mrefu hasa kwa wanunuzi,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad