HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 23, 2021

Watumishi wa Umma zingatieni Kanuni za Utumishi wa Umma

 

Adeladius Makwega, WHUSM-Dodoma

 Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema kuwa watumishi wa umma kama watazingatia kanuni za utumishi wa umma basi utumishi wa umma utafanyika kwa kiwango cha juu katika kuwapa huduma Watanzania katika sekta mbalimbali nchini.

 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wizarani hapo Bi Zahara Guga wakati akizungumza na watumishi wa wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.

 Akizitaja kanuni hizo; kutoa huduma bora, utii kwa Serikali, bidii ya kazi, kutoa huduma bora bila upendeleo, kufanya kazi kwa uadilifu, kuwajibika kwa umma pamoja na kuheshimu sheria na matumizi sahihi ya taarifa.

 “Panapokuwepo na matumizi sahihi ya taarifa ambayo ni miongoni mwa kanuni zetu za utumishi hapatokuwepo suala la kuvuja kwa siri za Serikali, jambo ambalo kama litazingatiwa linaweza kuzuia matatizo mengi ambayo yanaweza kumkumba mtumishi hadi kufukuzwa kazi” amefafanua Bi Guga.

 “Kwa nini mtumishi wa umma afike huku kubwa ni kutii sheria na kanuni zake tu si kingine” ameongeza Mkurugenzi Msaidiizi huyo wa Wizara ya Habari.

Kwa sasa taifa letu lina idadi ya watu inayokadiriwa takriban milioni sitini huku watumishi wa umma wakiwa ni laki tatu tu, na waumishi wa wizara hiyo ni wawakilishi wa Watanzania wengine. Aidha, Bi Guga amesisitiza watumishi hao wakumbuke wanawawakilisha watumishi wengine na wananchi ambao ndiyo wanaolipa kodi na fedha hiyo ndiyo inayotumika kulipa mishahara kwa watumishi wa Serikali.

“Suala la kufanyiwa kazi kwa siku mbili lifanyike kwa siku mbili na siyo mwezi mzima, hapo utakuwa umetimiza wajibu wako na umefanya kazi kwa bidiii na ukiwa mtumishi wa umma kuwajibika kwako ni wajibu na siyo hisani kwa wale wanaokuja kuhudumiwa” amesema Bi Guga.

 Wafanyakazi wa wizara hiyo mara baada ya kikao hicho wamesema kuwa vikao vya namna hiyo vifanyike mara kwa mara hatua itakayowapa watumishi nafasi ya kuuliza maswali na kujibiwa ili kusaidia kuondoa malalamiko yasiyo ya lazima.

“Hili ni juma la Utumishi wa Umma na tumejifunza mengi ninakumbuka awali niliwahi kuona maadhimsho ya utumishi wa umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja huko Dar es Salaam, kwa ujumla mimi binafsi nitaongeza juhudi katika kazi ili niweze kuwa mfanyakazi wa mfano bora huko mbeleni” alisema Julius Mgaya kutoka Idara ya Sera na Mipango ya wizara hapo.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad