Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU
wa mkoa wa Pwani,Aboubakar Kunenge amewapa salamu ,vishoka wa kuchochea
migogoro ya ardhi ,kuwa wakae mkao wa kuchukuliwa hatua kwani Pwani
kwasasa si salama kwao.
Pamoja
na hilo ,serikali ya mkoa imeamua kuunda timu maalum itakayosimamia
migogoro hiyo ili kupunguza malalamiko na kesi za ardhi .
Kunenge aliyasema hayo wakati wa mkutano wa baraza la biashara na uzinduzi wa baraza la biashara mkoa wa Pwani.
Alieleza ,kuna malalamiko ambayo yapo ndani ya uwezo wa mkoa kuyatatua ,lazima kuzingatia sheria na kufanya maamuzi .
"Serikali
inajipanga kumaliza maumivu kwa wale wenye kilio cha migogoro
isiyokwisha upande wa ardhi wakiwemo wawekezaji na wafanyabiashara na
wananchi "
"Ni lazima kuboresha mazingira ya biashara ili kuongeza pato hasa la mkoa na Taifa kijumla" aliongeza Kunenge.
Kunenge
alielezea ,viwanda vinajengwa ,lakini haileti mantiki kama vinajengwa
vingi kisha vinakufa ni bora kuviwekea mazingira bora ya uwekezaji
,kumaliza migogoro inayowazunguka kwa ustawi na maendeleo ya uwekezaji
na Taifa kijumla .
Alibainisha
,anahitaji kujua changamoto zao kila wilaya ,fursa zilizopo ikiwemo
EPZA na kuwepo Bandari wilaya ya Bagamoyo ili serikali iangalie namna ya
kuondoa vikwazo vilivyopo.
Mkuu
huyo wa mkoa aliitaka mamlaka ya mapato kuangalia na ya kuongeza walipa
kodi badala ya kuongeza kodi hali inayosababisha kukusanya mapato
hafifu.
Kunenge alitaka
taasisi kama TANROADS ,TANESCO na DAWASCO kujiwekea mipango kazi ya
kujua maeneo yenye mahitaji na ukubwa wa hitaji kila kiwanda ili
kuyamaliza.
Nae katibu mtendaji baraza la biashara
la Taifa ,dr. Godwil Wanga alifafanua kuwa , lengo la mabaraza ya
biashara ni kuleta majadiliano ya karibu kati ya sekta ya umma na sekta
binafsi.
Mwenyekiti wa
Chama Cha Wafanyabiashara ,wenye viwanda na kilimo ,Mkoa wa Pwani Saidi
Mfinanga alisema changamoto zinazowakabili wawekezaji na wafanyabiashara
na miundombinu mibovu ya barabara kutofikika maeneo yao husika ,ukosefu
wa umeme na maji ya uhakika.
Pia kodi isiyo rafiki kwa wafanyabiashara na mahusiano yasiyo mazuri kwa baadhi ya wakusanya kodi na walipa kodi.
No comments:
Post a Comment