HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 23, 2021

UZINDUZI WA NMB HEALTHCARE CLUB,SERIKALI YAIPONGEZA NMB

 

Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Klabu za afya ‘NMB Healthcare Club uliofanyka jijini Dar es Salaam

Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Aifelo Sichwale, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Klabu za afya ‘NMB Healthcare Club.
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa Klabu za afya ‘NMB Healthcare Club uliofanyka jijini Dar es Salaam.

………………………………………………………………..

Benki ya NMB, imekuwa ya kwanza nchini kuzindua Klabu za Afya ‘NMB Healthcare Club,’ mtandao unaowapa wadau wa Sekta ya Afya mikopo ya vifaa kazi, mitaji na uwekezaji, huduma inayokuja huku benki hiyo ikiwa imetumia zaidi ya Sh. Bilioni 32 kutoa mikopo kwa Sekta Binafsi ya Afya, kati ya Sh. Bilioni 112.5 ilizopanga kutumia hadi mwaka 2025.

NMB Healthcare Club imezinduliwa sambamba na Kongamano la Afya ‘Tanzania Health Summit 2021,’ uzinduzi uliowakutanisha wadau wa Sekta ya Afya zaidi ya 150, wakiwemo madaktari, wamafasia, wamiliki wa hospitali, zahanati, vituo na vyuo mbalimbali vya afya na viongozi wa vyama washirika.

Uzinduzi huo umefanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, ambako Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Aifelo Sichwale, aliipongeza NMB kwa kuwaunganisha na kuwapa uwezeshaji wadau muhimu wa Sekta ya Afya nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dk. Sichwale alibainisha kuwa, uzinduzi wa Klabu hiyo una baraka zote za Serikali na wanawaunga mkono NMB kwa juhudi zeo za kuwaunganisha Madaktari na wadau wengine muhimu wa Sekta ya Afya hapa nchini.

Dk. Sichwale aliipongeza NMB sio tu kwa kuwaunganisha wadau hao muhimu, bali utayari wao wa kutoa bure elimu juu ya fedha ambayo mahali pengine wangeipata kwa gharama kubwa, hasa inayohusu; uwekaji akiba, uwekezaji, umuhimu wa kupitisha fedha zao kwenye akaunti ya benki, pamoja na huduma zinginezo zitolewazo na NMB.

Naye Kaimu Afisa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa, aliwapongeza wadau wa Sekta ya Afya kwa kuona umuhimu wa Klabu hiyo na kuwaasa ambao bado hajajiung kufanya hivyo.

Aidha alibainisha kuwa NMB imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia sekta ya afya, ambako wanatoa misaada ya vifaa tiba, vikiwamo vinavyolenga kuhudumia eneo lenye changamoto nyingi, la afya ya uzazi. Aliongezea kuwa, NMB imeingia kwa nguvu moja kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana kwa wote, ambapo kupitia huduma ya Asset Financing – inayotoa mikopo nafuu mahsusi kwa Sekta Binafsi ya Afya,ambapo walitumia zaidi ya Sh. Bilioni 32 kufikia Machi mwaka huu, kati ya Sh. Bilioni 112.5 walizopanga kutumia hadi mwaka 2025.

NMB Healthcare Club ni uthubutu mwingine kutoka NMB unaowapa nguvu za ziada wawekezaji na wadau muhimu waliopo katika sekta hiyo

3 comments:

  1. You are really doing a marvelous job and keep the good work up and you have really inspired me.
    We are telecasting Hindi Reality Tv Show Bigg boss 15 free.Visit us to watch online its all episodes.
    bigg boss 15 voot bigg boss 15 voot online
    voot bigg boss 15 live

    ReplyDelete
  2. Youre so cool! I dont suppose Ive read anything in this way just before. So nice to seek out somebody by original ideas on this subject. realy we appreciate you starting this up. this excellent website is one area that is required on the internet, somebody with a little originality. helpful problem for bringing a new challenge on the internet! drug addiction treatment methods

    ReplyDelete
  3. Bigg Boss 15 Season Tv Show On Colors Tv that is Hosted By Sulman Khan in August 2021.This Show is Very Popular All Over the World.
    You Can Watch Bigg Boss 15 in Our Website in HD Quality.

    Bigg Boss 15 Today Watch Online
    Bigg Boss 15 Today Live
    Bigg Boss 15 Today Full Episode

    ReplyDelete

Post Bottom Ad