HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 14, 2021

Serikali, Wami ruvu zapigia chapuo utunzaji shirikishi rasilimali za maji

 


Na Mwandishi Wetu, Kilosa
WAKATI huu ambapo dunia inakabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ipo haja dhana ya utunzaji shirikishi wa vyanzo vya maji ikapewa kipaumbele ili kuokoa rasilimali hiyo muhimu kwa maisha ya binadamu.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kilosa, Cheyo Nkelege wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Jumuiya ya Watumia Maji katika Kijiji cha Msowero, ambapo ujenzi wake umesimamiwa na Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu.

Aidha, sambamba na mabadiliko ya tabianchi yanayotajwa kuhatarisha uhai wa rasilimali maji, changamoto nyingine inayotajwa ni ongezeko la shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo hivyo, zinazosababisha hali ya uchafuzi wa mazingira.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, Norah Mambya ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvi, alisema dhamira ya ujenzi wa ofisi ya Jumuiya ya watumaji maji katika eneo hilo utasidia ulinzi na uhifadhi endelevu wa rasilimali maji.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Msowero, wameelezea namna Jumuiya za Watumia maji zinavyosaidia kutunza na kulinda vyanzo vya maji katika eneo hilo.

Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Jumuiya ya Watumia Maji Katika Bonde Dogo la TAMI/MSOWERO wilayani Kilosa hadi kukamilika umegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 72.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kilosa, Cheyo Nkelege, akikata utepe kwenye Jiwe la Msingi kuashiria Ufunguzi rasmi wa Ofisi za Jumuiya ya Watumia Maji katik Bonde dogo la Tami/ Msowero Wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro.
Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, Elibariki Mmasi (Kulia) akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kilosa, Cheyo Nkelege wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Jumuiya ya Watumia Maji katika Kijiji cha TAMI/MSOWERO, ambapo ujenzi wa Ofisi hiyo umesimamiwa na Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kilosa, Cheyo Nkelege, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Msowero wakati wa Uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Jumuiya ya Watumia Maji katika Bonde dogo la Tami/Msowero Wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro.

Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji Bi Praxeda Paul, akizungumza wakati wa Uzinduzi huo, Waliokaa Meza Kuu Kutoka Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, (Kati) ni Kaimu mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kilosa Cheyo Nkelege ( wa tatu Kushoto) ni Bi Norah Mambya ambae ni Makamu Mwenyekiti Bodi ya Maji Bonde la Wamu Ruvu.





Baadhi ya Watumishi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu wakifuatilia tukio la Uzinduzi rasmi wa Ofisi za Jumuiya ya Watumia Maji katika Bonde dogo la Tami/Msowero wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro.





Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu Elibariki Mmasi akimuonesha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kilosa Cheyo Nkelege maeneo mbalimbali ya Ofisi za Jumuiya ya Watumia maji katika Bonde dogo la Tami/ Msowero Wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro.

Watumishi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu wakiwa katika Picha ya Pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kilosa, mara Baada ya kukamilisha kwa hafla ya Uzinduzi wa Ofisi za Jumuiya ya Watumia maji katika Bonde dogo la Tami/Msowero Wilayani Kilosa.




Wana Jumuiya ya Watumia maji katika Bonde dogo la Tami/Msowero wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu,mara Baada ya kukamilika kwa hafla ya Uzinduzi wa Ofisi za Jumuiya hiyo katika Kijiji cha Msowero Wilayani Kilosa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad