Rais Samia Suluhu Hassan atembelea na kukagua Daraja la JP Magufuli lenye Urefu wa Km 3.2 (Kigongo -Busisi) mkoani Mwanza - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 14, 2021

Rais Samia Suluhu Hassan atembelea na kukagua Daraja la JP Magufuli lenye Urefu wa Km 3.2 (Kigongo -Busisi) mkoani Mwanza

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) Eng. Patrick Mfugale ambaye alikuwa akielezea hatua za ujenzi wa Daraja la JP Magufuli lenye urefu wa Kilometa 3.2 linalounganisha kati ya Wilaya ya Misungwi na Sengerema mkoani Mwanza ambapo limefikia asilimia 27, huku Daraja la kupitisha vifaa likiwa limekamilika kujengwa kwa asilimia 100.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) Eng. Patrick Mfugale ambaye alikuwa akielezea jinsi ya kushusha nondo zilizosukwa katika umbo la duara katika mashimo marefu yaliyochimbwa ndani ya maji ya ziwa Victoria (haonekani pichani) leo tarehe 14 Juni, 2021.
Nondo zilizosukwa kwa umbo la duara zikishushwa ndani ya moja ya shimo refu lililochimbwa ndani ya maji ya ziwa Victoria katika hatua zinazoendelea za ujenzi wa Daraja la JP Magufuli lenye urefu wa Kilometa 3.2 Kigongo mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ujenzi wa moja na Nguzo ambayo imeshawekewa zege katika muendelezo wa kazi za ujenzi wa Daraja la JP Magufuli lenye urefu wa Kilometa 3.2 Kigongo mkoani Mwanza.
 
Ujenzi wa Daraja la kupitisha vifaa vya ujenzi ukiwa umekamilika kwa 100% huku ujenzi wa Daraja la JP Magufuli ukiendelea kwa kasi kubwa ambapo sasa umefikia asilimia 27.
Taaswira ya ujenzi wa Nguzo katika Daraja la JP Magufuli lenye urefu wa Kilometa 3.2 Kigongo mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia na wananchi wa Mkuyuni na Butimba Kona mkoani Mwanza wakati akielekea kuzindua miradi mbalimbali ya Maendeleo mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni 2021. PICHA NA IKULU


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad