RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA VIONGOZI KUAGA MWILI WA MAREHEMU MZEE CHRISANT MAJIYATANGA MZINDAKAYA MKOANI DAR ES SALAAM - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 9, 2021

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA VIONGOZI KUAGA MWILI WA MAREHEMU MZEE CHRISANT MAJIYATANGA MZINDAKAYA MKOANI DAR ES SALAAM

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho katika Jeneza lenye mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Marehemu Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya mara baada ya Misa ya kumuombea Marehemu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay mkoani Dar es Salaam leo tarehe 09 Juni 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiondoka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay mkoani Dar es Salaam mara baada ya kutoa Heshima za mwisho katika Jeneza lenye mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Marehemu Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya leo tarehe 09 Juni, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Misa ya kumuombea Marehemu Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay mkoani Dar es Salaam leo tarehe 09 Juni, 2021.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad