Henga: Mfumo dume ndio uliodidimiza wanawake kubaki nyuma katika uongozi - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 9, 2021

Henga: Mfumo dume ndio uliodidimiza wanawake kubaki nyuma katika uongozi

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya uongozi wanafunzi wasichana wa Vyuo Vikuu yaliyofanyika Chuo cha Usafirishaji (NIT) jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi Wajasiriamali wa Vyuo mbalimbali wakiwa na bidhaa zao katika Mafunzo ya uongozi yaliyofanyika Chuo cha NIT jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga akiangalia bidhaa mbalimbali zilizoandaliwa na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa wajasiriamali wakati Mafunzo ya uongozi kwa wasichana yaliyofanyika katika Chuoo cha NIT jijini Dar es Salaam.

Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) Paulina Tarazo kuhusiana na umuhimu wa Mafunzo ya uongozi kwa wasichana namna wanavyoweza kubadili mtazamo hasi na kuwa kuwa chanya.
Mjasirimali Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Happiness Michael akimhudumia Mwanafunzi mwenzake wa Chuo cha ustawi wa Jamii Zawadi Malombo walioshiriki Mafunzo ya uongozi.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MOJA ya changamoto ambayo imedidimiza wanawake wengi kutokushika nafasi mbalimbali za uongozi ni kutokana na mfumo dume ambao mwanamke ulimuweka kwa ajili ya kuwa mke wa mwanaume.

Hayo yamebainishwa na na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga wakati akifungua mafunzo kuhusu masuala ya kijinsia na haki za binadamu kwa wanafunzi wakike kutoka Vyuo Vikuu na kushiriki wanafunzi 400 mbalimbali nchini yaliyofanyika Chuo cha Usafirishaji (NIT) jijini Dar es Salaam.

Amesema changamoto ambazo zinawakwaza wasichana kufikia nafasi za uongozi ni mfumo dume uliopo, ambao pia unapelekea rushwa ya ngono kwa wanafunzi vyuoni na namna ambavyo wanalelewa katika familia zao ya kutojiamini katika kuweza kuongoza au kuwa sehemu ya maamuzi.

"Baadhi ya familia mtoto wa kike anaandaliwa kuwa mke na sio kiongozi, kwahiyo hii inawafanya wanakuwa wanabaki nyuma na kuona suala la uongozi anatakiwa kuwa mwanamme"amesema Henga.

Henga amesema mafunzo hayo ni kuwatia moyo watoto wa kike kuwa na chachu ya kuwania uongozi na kuona ni suala linalowezekana.

Henga ametoa wito kwa wasichana kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza na kuwania nafasi za uongozi kwani kila kitu kinawezekana na sio kuwaacha kwa ajili ya wanaume.

Aidha amesema wasichana wasimame kwa kujiamini kwa kufanya vizuri pamoja na kujifunza kwa wanawake wengine ambao wamekuwa viongozi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Binti Makini, Janeth John amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaandaa wasichana ili wawe viongozi wazuri, waliopikwa na waliotengenezwa na kwa kuja kuwa viongozi au kuwa sehemu ya maamuzi.

"Lakini pia uongozi unaendana na fedha hivyo tunawafundisha jinsi ya kujitegemea kwa kuwa wajasiriamali, kwahiyo ndo maana tumeweka mafunzo haya kuhakikisha tunawapika waweze kushika nafasi mbalimbali ili kuendana na vigezo vinavyotakiwa kukidhi pale anapokuwa kiongozi." Amesema Janeth.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad