DC Kanoni amuagiza mkurugenzi kutafuta fedha za kukamilisha ujenzi wa zahanati - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 11, 2021

DC Kanoni amuagiza mkurugenzi kutafuta fedha za kukamilisha ujenzi wa zahanati

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mkuu wa wilaya ya wanging'ombe mkoani Njombe Lauteri Kanoni amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo kutafuta fedha kiasi cha shilingi milioni kumi na kuzipeleka kijiji cha Katenge ili kukamilisha ujenzi wa zahanati unaotakiwa kukamilika tarehe 30 ya mwezi sita mwaka huu.

Ametoa agizo hilomara baada ya ziara yake ya kutembelea vijiji mbalimbali ikiwemo kijiji katenge,mambegu na samalia wilayani humo, kwaajili ya kukagua zahati ambazo zinajengwa mara baada ya serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni hamsini kwa kila kijiji,Mkuu wa wilaya hiyo amesema vijiji viwili Mambegu na samalia vimekamilisha ujenzi na ukarabati,lakini katenge ujenzi haujakamilika.

Katika ziara hiyo pia mkuu wa wilaya hiyo ya Wanging'ombe Lauter Kanoni ametembelea kata ya Saja ambayo imepokea fedha kiasi cha shilingi milioni mia tano kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya,na amewataka viongozi wa kata hiyo kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya miezi mitatu.

"Zhanati imeanza kujengwa kwa muda mrefu ujenzi upo karibu hatua za mwisho na fedha hazijatosha nimemuelekeza mkurugenzi kupitia mapato ya ndani waweze kutafuta hiyo fedha iliyobakia mpaka tarehe 30 zahanatia iwe imekamilika na wananchi waanze kupata huduma"alisema Kanoni

Diwani wa kata ya Wanging'ombe Geofrey Nyagawa amesema ujenzi wa zahanati ya Katenge upo hatua za mwisho kwa kuwa imeshaezekwa na kazi ya ukarabati inaendelea na kufafanua kuwa endapo watapewa fedha hizo ifikapo june 30 ujenzi huo utakua umekamilika kwa kila kitu.

"Tunataka tuikamiluishe hii zahanati ili wananchi waanze kupata huduma kwa sababu ni muhimu sana na wananchi wanasafiri umbali mrefu wa kilomita 23 kutoka hapa na tunamshukuru mheshimiwa mbunge hapa ametuletea milioni 50 ambazo tunaendelea kuzitumia"alisema Nyagawa

Hata hivyo mwenyekiti wa kijiji hicho Husen Nyamle na baadhi ya wananchi wamesema kuwa kukosekana kwa zahanati kijiji kwao kumewalazimu kutembea umbari wa kilomita 23 kufuata huduma za afya ambazo kwa sasa zinapatikana kituo cha afya Wanging'ombe

"Itakuwa na manufaa makubwa kawsababu kulikuwa na changamoto ya wengine kujifungulia njiani na usafiri wenyewe ni shida kwa kweli ni furaha sana kwa wana Katenge kupata Zahanati hii"aliseama Husen Nyamle  
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad