HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 22, 2021

BENKI YA EQUITY YAZINDUA KADI YA MALIPO YA EAZZY CARD

 

Mkuu wa biashara wa Equity Group Polycap Igathe pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Equity Bank (T) Esther Kitoka Wakionesha mfano wa kadi mpya ya "Eazzy Card" iliyo zinduliwa na benki hiyo Dar es Salaam. 22 June, 2021

Mkuu wa biashara wa Equity Group Polycap Igathe (kushoto) akishika kadi mpya "Eazzy Card" pamoja na viongozi wa Equity Bank (T) katika uzinduzi wa kadi hiyo mpya ya malipo uliofanyika Dar es Salaam. 22 June, 2021


***********************


Dar Es Salaam Tanzania,  22 June, 2021 Benki ya Equity (T) leo wamezindua rasmi kadi ya malipo ya awali ijulikanayo kama “Eazzy card” ikiwa na lengo la kurahisisha malipo ya kiditali na nchini kupitia huduma za fedha jumuishi.

 

Akizungumza katika  uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Serena,  Mkurugenzi Mwendeshaji wa Equity Bank (T) Esther Kitoka alisema,  kuwa kadi hiyo ni ya malipo ya kabla, ambapo mmiliki anaweza kutumia kiasi cha fedha ambacho tayari amekiingiza na kukitunza katika kadi yake husika.Kadi hii ni ya malipo ya awali hivyo inaruhusu kuwa na matumizi mengi ikiwemo kulipia ankara au bili, kununua bidhaa, kutoa pesa kwenye mashine za ATM na pia kufanya malipo ya mtandaoni.”


Kitoka alisema kuwa kufuatia kuzinduliwa kwa kadi hizo, kutawezesha hata watu wenye kipato cha chini kutunza fedha zao kwa urahisi na kujiwekea akiba kwa kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima. Alifafanua kwamba sasa wananchi wanaweza kupata kadi za Eazzy card kupitia Wakala wa Benki ya Equity au kupitia matawi ya Benki hiyo.

 

Pia ameeleza kuwa watanzania wengi wameonesha hamasa ya malipo ya kidigitali hivyo watahakikisha kuwa huduma hizo za kufanya malipo kwa njia ya mtandao zinawafikia wateja wao  na wana malengo makubwa mbeleni katika kujenga uchumi wa nchi hasa kwa  kwa kuzingatia sera ya nchi kwa sasa inayohamasisha na kuongeza kasi ya ukuaji wa malipo kwa njia ya kadi.

 

Akizungumzia juu ya faida ya kadi hizo Kitoka  alisema kuwa zinamuongezea mteja au asiye mteja Benki ya Equiy uwezo wa kufanya manunuzi pasipo kuwa na haja ya kubeba pesa taslimu. “Kuzipata kadi hizi sio lazima uwe mteja wa Benki ya Equity, pia ni rahisi kuziongezea salio kwa kupitia Wakala, Simu za Mikononi, matawini na kupitia huduma fedha kwa njia ya simu” alisema.

 

Naye Mkuu wa kitengo cha Malipo na Huduma mbadala wa benki hiyo Raph Ligalama ameeleza kuwa lengo la uzinduzi wa kadi hiyo ni pamoja na kurahisisha na kuwawezesha wateja na wasio wateja  wao kufanya (miamala) kidijitali na hivyo kuwaondolea usumbufu.

 

Faida za Eazzy card kutoka Equity Bank

 

·        Rahisi kufungua (Unahitaji kitambulisho cha NIDA tu)

·        Hakika na salama

·        Imeunganishwa na mtandao wa Visa hivyo kuweza kutumika kokote duniani

·        Urahisi wa kufanya malipo kwenye maduka, vituo vya mafuta, mahosipitali  Daladala na masokoni.

·        Huondoa ulazima wa kubeba fedha taslimu hivyo kupunguza hatari ya wizi au mahitaji ya chenji.

·        Rahisi kujaza fedha

·        Inatumia kokote duniani

·        Uwezo wa kuchukua pesa taslimu inapobidi (kupitia Wakala, ATM au tawi)

·        Uwezo wa kufanya malipo ya mtandaoni















No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad