Wizara
ya Maliasili na Utalii inakusudia kunyanga'nya maeneo yote ya Jumuiya
za Hifadhi za Wanyamapori za Jamii ambayo yatakutwa yamelimwa ikiwa ni
njia mojawapo ya kukabiliana na Wanyamapori wakali na Waharibifu .
Hatua
hiyo inakuja kufuatia baadhi ya wananchi na viongozi kufanya mashamba
na kuanza kulima mazao ya chakula katika Hifadhi hizo hali
inayopelekea Wanyamapori kama tembo kuacha kula nyasi na kulazimika
kutoka nje ya Hifadhi na kwenda kula mazao hayo.
Waziri wa
Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amesema hayo leo mapema Jijini
Dodoma wakati akizungumza na Watendaji wa Wizara hiyo kuhusu
changamoto zinazoikabili sekta ya Uhifadhi nchini hususan kwa Wananchi
wanaoishi kando kando mwa maeneo yaliyohifadhiwa.
Amesema kwa
mujibu wa sheria maeneo hayo ni mali ya vijiji na yanasimamiwa na
Serikali za Vijiji husika na mapato yatokanayo na Hifadhi hizo za Jamii
hutumiwa kwa ajili ya manufaa ya Wananchi ikiwemo kuboresha huduma za
kijamii kama vile shule na zahanati.
Amesema maeneo hayo ya
uhifadhi kusimamiwa na Serikali za vijiji ni ushirikishwaji wa Jamii wa
moja kwa moja ili kuiwezesha Jamii kufaidikana uhifadhi wa moja kwa moja
Amesema
hatua hiyo ya kunyang'anya itakwenda sambamba na upandishaji hadhi wa
Jumuiya hizo za Hifadhi za Wanyamapori za Jamii na kuwa Mapori Tengefu (
Game Controled Area) ambayo kwa mujibu wa Sheria Mamlaka ya Usimamizi
wa Wanyamapori (TAWA) ndiye atakayepewa kusimamia maeneo hayo.
Akizungumzia
hatua hiyo ya kunyang'anya Usimamizi kutoka Serikali za Vijiji na
kupelekwa TAWA, Dkt. Ndumbaro amesema kutatuma ujumbe mzito kwa Serikali
za Vijiji ambazo zinazosimamia Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori hizo
kuwa zimepewa jukumu la kusimamia Uhifadhi na sio vinginevyo.
Waziri
Dkt. Ndumbaro amesema kuna jumla ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori
zipatazo 22 na kati ya hizo ni Jumuiya za Wanyama[pori 10 pekee ndizo
zinafanya vizuri kimapato na kiuhifadhi.
Kufuatia hali hiyo,
amewataka Wakuu wa wilaya nchini ambao ndio Wenyeviti wa Jumuiya za
Hifadhi za Wanyamapori nchini kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele
kupiga vita shughuli zote za kibinadamu zinazofanyika katika maeneo hayo
ambazo haziendani na Uhifadhi.
'' Nina taarifa ya baadhi ya
Jumuiya hizo za Uhifadhi kuna Wakuu wa wilaya ambao ni Wenyeviti wa
kusimamia maeneo hayo nao wanalima katika maeneo, hadi kuna wengine
wameamua kufungua mashamba ya minazi katika maeneo ya Wanyamapori hili
halikubaliki'' amesisitiza Dkt. Ndumbaro.
Amesema kuna baadhi ya
Jumuiya za Hifadhi za Jamii za Wanyamapori zinazofanya vizuri na
zimekuwa zikikusanya pesa nyingi kutoka kwa Watalii ikiwemo Jumuiya ya
Hifadhi ya Wanyamapori ya Jamii ya Ikona ambayo kwa mwaka inapata bil.
2.6 zinazogawanywa kwa vijiji vitano pekee.
Ametoa wito kwa
Serikali za Vijiji kuhakikisha zinasimamia ipasavyo Uhifadhi katika
maeneo hayo kwa vile maeneo hayo ni utajiri mkubwa endapo kama
yatasimamiwa kwa ajili ya utalii na sio kugeuza kuwa mashamba.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Watendaji wa
Wizara ya Maliasili na Utalii leo Jijini Dodoma ambapo amesema shughuli
za Uhifadhi zinakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo baadhi ya Wananchi
na Viongozi kugeuza mashamba katika maeneo ya Wanyamapori hali
inayosababisha migogoro ya binadamu na Wanyamapori kuongezeka kila siku
hali inayotishia usalama wa Uhifadhi pamoja na maisha ya Wananchi
wanaoishi karibu na Hifadhi.
Wednesday, May 26, 2021

Home
HABARI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUNYANGA'NYA JUMUIYA YA HIFADHI ZA WANYAMAPORI ZA JAMII ZILIZOGEIZWA KUWA MASHAMBA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUNYANGA'NYA JUMUIYA YA HIFADHI ZA WANYAMAPORI ZA JAMII ZILIZOGEIZWA KUWA MASHAMBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment