NHIF na BENKI YA CRDB WABORESHA MAISHA YA WAKULIMA KUPITIA MPANGO WA USHIRIKA AFYA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 31, 2021

NHIF na BENKI YA CRDB WABORESHA MAISHA YA WAKULIMA KUPITIA MPANGO WA USHIRIKA AFYA

Benki ya CRDB na Mfuko wa Bima ya Taifa NHIF imeendelea na utekelezaji wa tumeanza utekelezaji wa mpango wa “Ushirika Afya” kwa  kuingia makubaliano na Chama Kikuu cha Ushirika cha maziwa mkoani Tanga kwa ajili ya kuwapatia bima ya afya wanachama wake mkoani humo ambao ni wazalishaji wa maziwa kama sehemu ya mpango wa Ushirika Afya.

Mgeni Rasmi wakati wa Kuingia Makubaliano hayo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mh. Thobias Mwilapwa amewapongeza benki ya CRDB na Mfuko wa Bima ya afya ya Taifa kwa Ubunifu wa mpango huo ambao utawafaidisha wakulima wengi nchini “ Nasihi wanaushirika katika mkoa wa Tanga Kutumia Fursa hii tujiunge kwa wingi kwenye vyama vya ushirika ili kutumia fursa hii kuboresha maisha ya familia zetu” Mh. Mwilapwa
Kwa niaba ya Benki ya CRDB Afisa Biashara Mkuu  Dkt. Joseph Witts alisema Katika Makubaliano hayo Benki ya CRDB itawawezesha wanachama wa chama kikuu kulipia bima ya Afya bila riba yoyote na hivyo kuboresha uzalishaji wa maziwa katika mkoa wa Tanga.” Huu ni mpango maalumu wa Benki yetu unaolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya katika maisha ya wateja wetu walioko kwenye sekta ya Kilimo nchini kote” alieleza Dkt. Witts.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa NHIF Bw. Christopher Mapunda alisema kuwa mfuko wa Bima ya taifa katika mkakati huu unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya kwa wakulima na wafugaji nchini. “Mpango utawawezesha wazalishaji wa maziwa kupata huduma za afya katika vituo zaidi ya Elfu nane katika nchi nzima” alieleza Bw. Mapunda
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa maziwa mkoani Tanga Nd. Shamte Said amewashukuru Benki ya CRDB na NHIF kwa kuja na mpango huo “ Nawapongeza kwa kuwakumbuka wazalishaji wa maziwa nawahidi tutatumia fursa hii kujihakikishia upatikanaji wa matibabu” Ndg. Shamte

Hafla ya utiaji sahihi wa makubaliano hayo ulihudhuriwa na Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga, Maafisa wa Mfuko wa Bima ya Taifa, Maafisa wa Benki ya CRDB na Wajumbe Wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika wa Maziwa Tanga.

Utekelezaji wa mpango wa Ushirika Afya ulianza mapema wiki iliyopita ambapo Benki ya CRDB na NHIF waliingia mkataba wa makubaliano na na vyama vya ushirika vya CHUTCU kilichopo wilaya ya Chunya, vyama vya MCU na MWAMARU vilivyopo wilaya ya Rungwe, Mbeya.
Katika mpango huu Benki ya CRDB inasidia kurahisisha upatikanaji wa bima za afya kwa wakulima waliopo katika vyama vya ushirika (AMCOS) kupitia huduma ya mkopo wa gharama za bima iliyopewa jina "Ushirika Afya Premium Loan." Huduma hiyo inatolewa bila makato wala riba. Mkulima anaruhusiwa kukata bima yake, pamoja na wategemezi wake ikiwamo mke/ mume na watoto.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad