Mama Sekita Nsekela atoa mkono wa Idd kwa kituo cha Watoto cha TanKids, Gongo la Mboto - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 13, 2021

Mama Sekita Nsekela atoa mkono wa Idd kwa kituo cha Watoto cha TanKids, Gongo la Mboto

Mke wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mama Sekita Nsekela (wa pili kulia) akikabidhi kwa Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha kulea Watt wenye uhitaji (Yatima) cha TanKids kichopo Gongo la Mboto, Christian Kiponda (wa tatu kulia), mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni tatu (3,000,000/-)  pamoja bidhaa za chakula na magodoro ikiwa ni sehemu ya sadaka ya Mkono wa Idd kwa watoto wa kituo hicho, kwenye Makao Makuu yao, eneo la Markaz, Gongo la Mboto, Dar es salaam leo. Wengine pichani kutoka kulia ni Afisa wa Beki ya CRDB. Wema Mwamunyange, Katibu wa Kituo hicho, Charles Wambura, pamoja na baadhi ya watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.Mke wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mama Sekita Nsekela (wa pili kulia) akikabidhi kwa Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha kulea Watoto wenye uhitaji (Yatima) cha TanKids kichopo Gongo la Mboto, Christian Kiponda (wa tatu kulia), moja ya ndoo zenye sabuni ikiwa ni sehemu ya sadaka ya Mkono wa Idd kwa watoto wa kituo hicho, kwenye Makao Makuu yao, eneo la Markaz, Gongo la Mboto, Dar es salaamMama Sekita Nsekela akiangalia moja ya vitanda wakati alipotembelea vyumba vya kulala watoto hao kituoni hapo.Mama Sekita Nsekela akiwa katika mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha kulea Watoto wenye uhitaji (Yatima) cha TanKids kichopo Gongo la Mboto, Christian Kiponda.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad