HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 1, 2021

ECOBANK TANZANIA YATOA ELIMU KWA WANANCHI NA WAFANYABIASHARA KANDA YA ZIWA

 Ecobank Tanzania imeendelea na kampeni ya kuingia mtaani ya kutangaza huduma na kazi zinazotolewa na Benki hiyo katika Mkoa wa Mwanza pamoja na mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa, May 28 hadi 30, 2021.

Benki hiyo imejikita kutoa Elimu kwa wateja wao wa ambao ni Wafanyabiashara wa Kati, wa wadogo na wakubwa pamoja na wale ambao sio wateja wao kuhusu huduma za Kibanki zinazotolewa na Benki hiyo ili kuweza  kupanua wigo wa ufahamu hasa kwenye kutunza  akiba, huduma zitakazitolewa ni pamoja na elimu ya Mkopaji na jinsi ya kupata mkopo kwa riba nafuu.

Elimu hiyo pia imetolewa kwa Wafanyabiashara hao kuhusu Akaunti za Benki hiyo ambazo ni (Current Account, Savings Account, Express Account, Termed Diposit Account).

Ecobank Tanzania inaendelea kuunga mkono mikakati ya Serikali ya kuongeza tija katika sekta ya huduma za fedha na kupanua huduma hizo ili kuwafikia watanzania walio wengi na ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki.

Pia Benki hiyo imetoa shukrani kwa wananchi waliotoa muda wao kusikiliza  huduma

Wananchi wakisoma vipeperushi vya Ecobank Tanzania vyenye elimu kuhusu kazi zinazofanywa na benki hiyo wakati wa kampeni ya mtaa kwa mtaa ili kuunga mkono mikakati ya Serikali ya kuongeza tija katika sekta ya huduma za fedha
Mkuu wa kitengo cha SME kutoka Ecobank Tanzania, Juma Hamisi akitoe elimu kwa mfanyabiashara katika jiji la Mwanza wakati wa kampeni ya kuingia mtaani ya kutangaza huduma na kazi zinazofanywa na benki hiyo.
Baadhi ya watu wa mauzo wakitoa elimu na kugawa vipeperushi vya kazi zinazofanywa na Ecobank Tanzania wakati wa kampeni ya mtaa kwa mtaa iliyofanyika katika mkoa wa Mwanza na mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Sumalu(kulia) akiwa studio za Radio Free Africa kwa ajili ya kurekodi matangazo yatakayoweza kuwafikia wananchi wengi wakai wa kampeni ya Benki hiyo iliyofanyika Mkoani Mwanza.
Kampini ya kuhamasisha wananchi kujua kazi pamoja na huduma zitolewazo na benki hizo ukiendelea


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad