Afisa
Mkuu Uendeshaji wa Benki ya CRDB Bwana Bruce Mwile (Katikati) wakati wa
mjadala uliolenga kuangalia mchango wa Teknolojia katika kuendeleza
uchumi wa Kidigitali kulia na kushoto kwake ni wadau wa sekta na
Taasisi nyingine.
Na Mwandishi Wetu.
Benki ya CRDB imeshiriki katika Wiki ya Uvumbuzi kwa Mwaka huu 2021 , Mada kuu ya mwaka huu ni “Ubunifu kwa Uchumi wa Kidijitali Stahimilivu na Jumuishi ( Innovation for a Resilient and Inclusive Digital Economy ) ”.
Wiki ya Ubunifu Tanzania imekua kwa kasi kutoka mwaka 2015 ikiwa na wahudhuriaji karibu 500 hadi mwaka jana, 2020 ilipoudhuriwa na zaidi ya watu takribani 7,000 na kuwa ya kitaifa zaidi. Wiki hii imetoa jukwaa kwa wabunifu wengi kuonekana, wadau zaidi kuunda ushirikiano wa maana, maarifa mengi ya kushirikishwa, mipango mingi ya ubunifu itakayoonyeshwa na masuala muhimu yanayohusiana na sera kujadiliwa.
"ukiangalia zipo fursa nyingi sana katika Benki yetu ya CRDB, katika Uvumbuzi tunaoufanya tunawajali watu wote hata wamachinga, walimu, watoto na hata sekta mbalimbali, na ukitaka kujua kwamba sisi ni Benki inayosikiliza wateja juzi tulizindua simu Banking na watu wakatoa maoni kwamba tupunguze makato na tulifanya ivyo" Alisema Bwana Bruce Mwile.
No comments:
Post a Comment