BENKI YA EQUITY TANZANIA YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA JIJINI MWANZA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 3, 2021

BENKI YA EQUITY TANZANIA YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA JIJINI MWANZA

Benki ya Equity(T) imekutana na Wateja wake na Wafanyabishara wa mkoani Mwanza  kuwajengea uwezo wa kibiashara, kufangulia fursa za uwezeshaji walizonazo na pia kuelezea kuhusu muelekeo na muanekano wake mpya.

Warsha hiyo ilifanyika April 29, 2021 ikihusisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali mkoani Mwanza waliojengewa uwezo kuhusu masuala ya kifedha ikiwemo mbinu za utunzaji fedha, namna ya kukuza mtaji na kushirikiana ili kukua pamoja kibiashara.

Akifungua warsha hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi alisema Serikali inaendelea kuwawekea mazingira rafiki wajasiriamali na wafanyabiashara ili kufanya biashara zao ili kuongeza pato la taifa.

"Naipongeza Benki ya Equity kwa kuundaa hafla hii ya kuwakutanisha wateja wake. Serikali inatambua na kuthamini sana mchango wenu katika kukuza uchumi wa Mkoa wetu na nchi kwa ujumla. Mwanza ni kiungo muhimu sana kwa uchumi wa Taifa kwa kuwa na vivutio vya utalii, madini, mazao ya Ziwa Victoria, kilimo cha pamba, chakula na mazao ya ufugaji. Hivyo uwepo wa Benki imara kama Equity ni suala la msingi sana ili kuhakikisha tunapata maendeleo" alisema Dkt. Nyimbi.
Kwa upande wake  Mkurugenzi Mwendeshaji wa  Benki ya Equity (T) Esther Kitoka aliwahimiza wajasiriamali na wafanyabiashara nchini kuchangamkia huduma za kifedha zitolewazo na Benki hiyo ili kuongeza tija. "Nawakaribisha Equity Bank kuwa ndiyo benki yenye riba nafuu huku ikiwa haina makato kabisa katika huduma zake nyingi, Benki ya Equity pia inatoa mikopo nafuu kabisa sokoni. Karibuni tuwahudumie” alisema Bi.Kitoka.
 
Bi.Kitoka pia Amesema benki hiyo imeendelea kutanua na kuboresha huduma zake ikiwemo uwepo wa Matawi, vituo vya kutolea huduma, Mawakala wa Benki na Mashine za kutolea fedha yaani ATMs. Aidha amesema kwa mkoa wa Mwanza Pamoja ya kuwa na tawi kubwa na la kisasa, Benki ya Equity vituo vya huduma yaani Merchants 114, wateja zaidi ya elfu hamsini Mawakala zaidi ya 600, huku llikiwa limetoa mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni 50 katika sekta mbalimbali kama Kilimo, Viwanda, Utalii, Usafirishaji na uzalishaji mwingine.
‘’Nina furaha pia kuwajulisha kuwa katika kuunga mkono sera ya uchumi wa bluu na kuongeza uzalishaji wa mazao ya bahari na maziwa, Benki ya Equity imeshatoa zaidi ya shilingi bilioni moja kwa hapa Mwanza tu, kwa zaidi ya wavuvi binafsi na vikundi 200 vya uvuvi ili kuongeza tija katika ufugaji na uvunaji wa samaki” alisema.

Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo, Meleck Sadick pamoja na John Mtimwa wameipongeza benki ya Equity kwa namna ilivyowawezesha kwa njia ya mikopo na kuinua biashara zao ambapo wameomba benki hiyo kuendelea kuboresha zaidi huduma zake ili kuwanufaisha wafanyabiashara wengi zaidi.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi akizungumza na Mkurugenzi Mwendeshakji wa Benki ya Equity (T) Esther Kitoka katika hafla iliyoandaliwa na wateja wa Benki mkoani Mwanza hivi karibuni.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad