HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 24, 2021

WAZIRI MHAGAMA ATOA MWONGOZO WA UTENDAJI KAZI KWA MAMENEJA NSSF

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akizungumza na  Mameneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kutoka mikoa mbali mbali, Leo Jumamosi 24/04/2021. Dar Es Salaam 
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Prof. Jamal Adam Katundu akitoa salamu na kumkaribisha waziri Mhe. Jenista Mhagama, kwenye kikao cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama na  Mameneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Leo Jumamosi 24/04/2021, Dar Es Salaam. 
  
 Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, akitoa ahadi kwa kusema NSSF itaendelea kua kua kwa kasi na kutimiza kile ambacho Serikali yetu na Rais wetu anakitegemea, katika kikao cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama na  Mameneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Leo Jumamosi 24/04/2021, Dar Es Salaam.

Kushoto ni Waziri  wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiwa na
Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, katika kikao cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama na  Mameneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Leo Jumamosi 24/04/2021, Dar Es Salaam.


***************************


 Awataka kutoa ushirikiano kwa Serikali ya awamu ya sita.
 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mh. Jenista Mhagama amewataka Mameneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kufanya kazi kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uaminifu na kila mmoja kusimama kikamilifu katika nafasi yake na kutekeleza wajibu wake.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kilichomkutanisha na Mameneja wa NSSF kutoka Mikoani Jenista amesema, kikao hicho kimelenga kubaini na kuelekezana hatua za kupunguza au kuondoa mapungufu katika masuala ya uendeshaji wa mfuko huo na kutekeleza majukumu ya mfuko huo kwa ufanisi na weledi zaidi.

"Mara nyingi nimeongea na wajumbe wa bodi pamoja na  menejimenti kusisitiza masuala yanayotuhusu ila leo nimeamua kushuka chini na kuongea na Mameneja ili msikie maelekezo kwa kuwa mwelekeo wetu wa sasa ni kusimamia kwa dhati masuala yote ya uendeshaji I'll kuhakikisha mfuko unatekeleza kwa weledi majukumu yake." Amesema.

Waziri Mhagama amesema, Majukumu ya msingi ya mfuko huo ni pamoja na kusajili wanachama na waajiri, kukusanya michango, kuwekeza kwa tija ili kuleta faida la kulipa mafao bora bora kwa wanachama wake.

"Mwaka 2018 tulipiga hatua kubwa ya kufanya maboresho kwenye sekta ya hifadhi ya jamii kwa kuunganisha mifuko ili kuleta maboresho ya huduma, kupunguza gharama na kuleta ustahimilifu na tuna mifuko miwili ambayo ni NSSF na PSSSF yenye dhima ya kufikia malengo kutoa huduma endelevu za hifadhi ya jamii." Amesema.

Aidha amesema bado kuna changamoto ambazo kama mfuko wanatakiwa kuzifanyia kazi ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

" Hadi sass waajiri na wafanyakazi waliopo kwenye sekta binafsi na sekta isiyo rasmi ambao bado hawajasajiliwa na NSSF, ni vyema mkatoa elimu na hamasa ili kushawishi walio nje ya wigo kujiunga, nawaelekeza kuja na mkakati wa uhamasishaji na utoaji elimu, watendaji wa mikoa msikae ofisini waende maeneo ya pembezoni kwa mazoezi ya usajili, mboreshe huduma za usajili kwa kupunguza gharama na kuanzia sasa wizara itaanza kuchukua hatua kwa watendaji wa mikoa na  wafanyakazi wanaofanyishwa kazi bila kusajiliwa kwenye mfuko." Amesema.

Kuhusiana na kufanya kaguzi kwa waajiri Waziri Mhagama amesema,kumekuwa na uzembe kwa baadhi ya watendaji kuzembea kufanya kaguzi hizo na kuwaelekeza kuzingatia ukaguzi wa mara kwa mara na Wizara itafanya hivyo hata kwa kushtukiza  na Serikali itahusisha vyombo vingine katika kuwafuatilia watendaji wa mikoani wanaojihusisha na rushwa na kuwachukulia hatua.

Pia amewata kukukusanya michango kwa wakati kwa ili kudhibiti ukuaji hafifu wa mfuko na kuwataka watendaji kusimamia sheria na miongozo yenye kulinda maslahi ya wafanyakazi na hiyo ni pamoja na kusimamia utaratibu wa kulipa mafao.

Vilevile ameelekeza kuzingatia utoaji wa huduma bora na kulinda maslahi ya wanachama kwa kuondoa malalamiko ya huduma duni naa kuutaka mfuko huo kujenga utamaduni wa ufuatiliaji na kutopuuza malalamiko ya wanachama.

Waziri Mhagama amewataka pia kupima utendaji wao wa Kazi na ufikiaji wa malengo ya kimakakati, kufanya mapitio ya mpango mkakati ili kuona uhalisia wa malengo waliojiwekea pamoja na kuwa waadilifu, wazalendo na kuzingatia maadili ya utumishi na kuielekeza bodi Bodi na Menejimenti ya mfuko kusimamia kwa karibu suala la maadili kwa watumishi.








No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad