KAMPUNI YA CANOPUS YASAINI MAKUBALINO YA USAMBAZAJI WA ZANA ZA KILIMO NCHINI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 19, 2021

KAMPUNI YA CANOPUS YASAINI MAKUBALINO YA USAMBAZAJI WA ZANA ZA KILIMO NCHINI

 Kampuni ya CANOPUS ni kampuni ya Kwanza  hapa nchini kusaini Mkataba wa makubaliano mikataba wa makubaliano wa kusambaza zana za kilimo na mashine bora pamoja na kutoa huduma za kiufundi, mafunzo, ushauri na matengenezo pale zinapohitajika na wateja kutoka kampuni ya PASS Leasing.


Canopus Agro ni kampuni ya kitanzania inayolenga kuwahudumia wakulima, wafugaji, wavuvi na wenye viwanda. Kampuni hii inasambaza na kuzalisha mashine bora zaidi, zana bora zaidi, pembejeo na huduma. 

Bidhaa zetu zinajumuisha aina zaidi ya 130 za mashine na vifaa vinavyokidhi changamoto na mazingira ya Kitanzania pamoja na mahitaji yote ya kiufundi kulingana na Kituo cha Kilimo, Mitambo na Teknolojia ya Vijijini (CAMARTECH) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS)

 Mkurugenzi Mtendaji PASS Leasing, Killo Lusewa na Mkurugenzi wa CANOPUS, Godwin Msigwa wakibadilishana mikataba wa makubaliano wa kusambaza zana za kilimo na mashine bora pamoja na kutoa huduma za kiufundi, mafunzo, ushauri na matengenezo pale zinapohitajika na wateja. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za PASS Leasing leo Aprili 19, 2021 Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa CANOPUS, Godwin Msigwa kugonga mhuri mkataba wa makubaliano wa kusambaza zana za kilimo na mashine bora pamoja na kutoa huduma za kiufundi, mafunzo, ushauri na matengenezo pale zinapohitajika na wateja, wa kwanza kulia ni Afisa mwandamizi, uwezeshaji PASS Leasing, Maria Wambura, wa kwanza kushoto ni Col. Mwanasheria Aloyce Laiser (Rtd) na wapili kutoka kushoto ni Maneja Mawasiliano PASS TRUST, Bevin Bkoke.

Mkurugenzi Mtendaji PASS Leasing, Killo Lusewa na Mkurugenzi wa CANOPUS, Godwin Msigwa wakisaini Mkataba wa makubaliano wa kusambaza zana za kilimo na mashine bora pamoja na kutoa huduma za kiufundi, mafunzo, ushauri na matengenezo pale zinapohitajika na wateja. Mkataba huo umesainiwa leo Aprili 19, 2021 Mkoa wa Dar es Salaam, wa kwanza kulia ni Afisa mwandamizi, uwezeshaji PASS Leasing Bi. Maria Wambura, wa kwanza kushoto ni Mwanasheria wa CANOPUS Col. Aloyce Laiser (Rtd) na wapili kutoka kushoto ni Maneja Mawasiliano PASS TRUST, Bevin Bkoke.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad