Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mheshimiwa Jenista Mhagama akikabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza kwa Taasisi za Fedha kwa Mkuu wa Idara ya Ulinzi, Usalama na Afya mahala pa kazi wa Benki ya CRDB Missana Mutani katika maadhimisho ya siku ya Ulinzi, Usalama na Afya Mahala pa kazi yaliyofanyika tarehe 28/04/2021 uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Benki ya CRDB imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Ulinzi, Usalama na Afya mahala pa kazi inazingatiwa kwa wafanyakazi wake. Haya yamedhihirishwa katika maadhimisho ya siku ya Ulinzi, Usalama na Afya mahala pa kazi Duniani yaliyofanyika kuanzia tarehe 26/04/2021 hadi tarehe 28/04/202 katika viwanja vya nyamagana Jijini Mwanza yaliyohusisha Taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.
=========
Katika maadhimisho hayo Benki ya CRDB iliibuka mshindi kwa kushika nafasi ya kwanza kwa taasisi za fedha zinazozingatia Ulinzi, Usalama na Afya mahala pa kazi nchini.
Matokeo hayo ni matunda ya jitihada zinazofanywa na Benki ya CRDB katika kuhakikisha wafanyakazi wake wanatimiza majukumu yao katika mazingira safi na salama. Miongoni mwa jitihada zilizofanywa na Benki ya CRDB ni kuanzisha kitengo maalum kinachosimamia na kushughulikia maswala ya Ulinzi, Usalama na Afya mahala pa kazi.
Vilevile kuanzishwa kwa mfumo maalum wa osha ujulikanao kama “OSHA SYSTEM” ili kurahisisha ufikishaji wa taarifa zinazohusu mazingira bora ya utendaji kazi. Hatua hizi zimepelekea Benki ya CRDB si tu kuendana na kufuata sheria za mamlaka husika bali imekua ni sehemu ya utaratibu wa ndani wa Benki kwa wafanyakazi wake yaani “Moral Obligations”.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa Idara ya Ulinzi, Usalama na Afya mahala pa kazi Missana Mutani alisema mafanikio ya kibiashara ya Benki ya CRDB yanatokana na mazingira bora kwa wafanyakazi yanayowawezesha kufanya kazi kwa usalama na kuleta hamasa katika uzalishaji.
“Benki ya CRDB tumejipanga kuhakikisha wafanyakazi wetu wanaepukana na changamoto za maradhi mbalimbali hasa yasioambukizwa kama ulemavu unaotokana na mazingira hatarishi ya kufanyia kazi, hivyo tulianza kwa kuhakikisha tunaweka mikakati madhubuti ikiwemo kutenga fedha za kutosha kuwezesha utekelezaji wa jitihada hizi” alisema Missana.
No comments:
Post a Comment