ZIARA YA KUKAGUA MRADI WA MAJI WA BILIONI 520 WILAYA YA ARUSHA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 2, 2021

ZIARA YA KUKAGUA MRADI WA MAJI WA BILIONI 520 WILAYA YA ARUSHA

 Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mheshimiwa Kenani Kihongosi amefanya ziara ya kikazi Kukagua meadi wa Maji wa Bilioni 520 akiambatana na Madiwani wa jiji la Arusha wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jijibla Arusha Mheshimiwa Maximillian Iraghe pamoja na watendaji wa kata katika Jiji la Arusha.

Mheshimiwa mkuu wa Wilaya Amewaeleza Madiwani  pamoja na watendaji kata kwenda na Kuwafafanulia wananchi Hatua nzuri ya Mradi ilipofikia na wawaeleze wananchi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dr. JOHN POMBE MAGUFULI  Ipo Kazini kuhakikisha maendeleo makubwa yanawanaufaisha wananchi.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewapongeza Mamlaka ya Maji  AUWSA na Kuwaagiza wakamilishe mradi kwa wakati ili Wananchi wafurahie Matunda ya Serikali yao.

Mkuu wa Wilaya pamoja na Madiwani na watendaji wa kata wamemshukuru Mheshimiwa Rais DR JOHN POMBE MAGUFULI kwa kutoa fedha nyingi katika mradi huo na wamemuombea kwa Mwenyezi Mungu azidi KUMPA Nguvu na Afya Katika kuwatumikia WATANZANIA.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad