WAZIRI MKENDA ATOA TATHMINI YA KAZI KUWADHIBITI NZIGE WA JANGWANI WALIOVAMIA NCHINI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 2, 2021

WAZIRI MKENDA ATOA TATHMINI YA KAZI KUWADHIBITI NZIGE WA JANGWANI WALIOVAMIA NCHINI

 

 

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akiongea na Waandishi wa Habari mjini Moshi ambapo amesema makundi ya nzige yameendelea kudhibitiwa na kuwa hakuna madhara yaliyojitokeza kwenye mashamba ya wakulima hadi sasa (Picha na Wizara ya Kilimo)

…………………………………………………………………………………………………….

Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda (Mb) ametoa tathmini ya kazi ya kuwadhibiti nzige wa jangwani waliovamia nchini mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu na kuwa hadi sasa wamedhibitiwa na wataalam wa Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana  na halmashauri za wilaya za Longido, Siha na Simanjiro.

Prof. Mkenda ameeleza hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari Moshi mkoani Kilimanjaro kuwa mapambano dhidi ya nzige yanaendelea vizuri na kuwa hadi sasa hakuna madhara yoyote kwenye maeneo ya kilimo na mifugo ya wananchi na kuwa jitihada za kuangamiza makundi  yaliyobakia zinaendelea kwa kutumia helkopita na mabomba ya kupiliza kwa mikono.

“Tupo makini kuwakabili nzige hadi sasa hatujapata madhara yoyote kwa mashamba ya wakulima hivyo watanzania wasiwe na taharuki “alisisitiza Prof. Mkenda.

Kuhusu mikakati ya kupambana na nzige Waziri Mkenda amesema hadi leo tarehe 01 Machi tayari kuna helkopta kutoka Shirika la Nzige Wekundu (RLCO) na kuwa serikali itaongeza ndege ya pili kutoka shirika la Nzige wa Jangwani (DLCO) kupulizia makundi madogo ya nzige walionekana maeneo ya wilaya za Longido kufuatia uwepo wa taarifa kuwa nzige wachanga kutoka Kaunti ya Machakos nchini Kenya wanaweza ingia Longido.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad