HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 8, 2021

RC TABORA ATOA ONYO KWA WAVAMIZI WALIOBAKI KATIKA HIFADHI YA MSITU WA ISAWIMA WILAYANI KALIUA


 

 
Mkuu wa Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi, Brigedia Jenerali Julius Gambosi (aliyenyoosha mikono na kushika fimbo) akitoa maelezo mafupi jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( mwenye suti ya drafti) kuhusu zoezi la utangulizi la kijeshi lililo kuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.
 
Mkuu wa Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi, Brigedia Jenerali Julius Gambosi (aliyenyoosha mikono na kushika fimbo) akitoa maelezo mafupi jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( mwenye suti ya drafti) kuhusu zoezi la utangulizi la kijeshi lililo kuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.
 
Mkuu wa Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi, Brigedia Jenerali Julius Gambosi (aliyeshika fimbo) akimuongoza jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( mwenye suti ya drafti) kuelekea eneo mojawapo  la zoezi la utangulizi la kijeshi lililo kuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.

 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( mwenye suti ya drafti) akisalimiana jana na Maafisa wa Jeshi la Wananchi kutoka Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi alipohudhuria kusitisha kwa zoezi la utangulizi la kijeshi lililo kuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.
 
Mkuu wa Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi, Brigedia Jenerali Julius Gambosi akimkabidhi jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( mwenye suti ya drafti) Bendera ikiwa ni ishara ya kumalizika kwa zoezi la utangulizi la kijeshi lililokuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.

 
Mkuu wa Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi, Brigedia Jenerali Julius Gambosi akimuonyesha jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( mwenye suti ya drafti) mmoja ya mabomu ambayo walikuwa wakiyatumia katia zoezi la utangulizi la kijeshi lililokuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.

 
Wapiganaji  Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi, wakilipua mabomu jana wakati wa zoezi la utangulizi la kijeshi lililokuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.

 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( mwenye suti ya drafti) akiangalia mmoja mzinga wa kurusha mamomu wakati wa kuhitimisha  zoezi la utangulizi la kijeshi lililokuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.
 
Mkuu waMkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( katikati mwenye suti ya drafti) akishiriki mazoezi jana na Maafisa wa Majeshi na Wapiganaji kutoka Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi kabla ya kumalizika kwa zoezi la utangulizi la kijeshi lililokuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.

 
Wapiganaji kutoka Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi wakirudi katika eneo la Kambi ya muda baada ya kumalizika jana kwa zoezi la utangulizi la kijeshi lililokuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.

Picha na Tiganya Vincent

 

 

NA TIGANYA VINCENT

VIKUNDI vya watu waliovamia na kubaki katika eneo la Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima lilipo wilayani Kaliua ambao wanaendelea kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji wametakiwa kuondoka kwa hiari kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati wakati akihitimisha zoezi la utangulizi la kijeshi lililo kuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.

Alisema Serikali imeamua kuchukua hatua baada ya kuona kuwa uvamizi katika eneo hilo unaendelea na kutishia uendelevu wa ziwa Tanganyika na kupoteza maisha ya baadhi ya wananchi na watendaji.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema Serikali haiwezi kuendelea kuwacha wavamizi waendelee la uharibifu ambao utaishia ikojia ya eneo hilo ambalo ni muhimu kwa ajili ya upelekaji wa maji ziwa Tanganyika na mapito ya wanyama kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Mto Ugalla, Mbuga ya Kigosi Moyosi na Mpanda line.

Alisema Serikali ya Mkoa wa Tabora na Wilaya ya Kaliua wametumia Diplomasia na kutoa elimu ya kutosha kilichobaki watu wote waliomo katika msitu kuondoa wao wenyewe kwa hiari yao.

Dkt. Sengati aliwataka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuhakikisha baada bya kazi iliyofanywa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika eneo wavamizi wasiingie tena na kuharibu maliasi ikiwemo ukataji magogo na uwindaji haramu wa wanyamapori unaofanyika katika eneo hilo.

Aliwataka kufanyakazi kwa kuzingatia maadili na sharia katika kuhakikisha wavamizi wote na vikundi vyote vya uhalifu vilivyomo ndani ya msitu huo vinaondoka ili uharibifu usiendelee.

Alisema lengo la Serikali ni kutaka msitu huo hatimaye uje upande kwa ajili ya kuongeza mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua na Taifa kwa ujumla.

Naye Mkuu wa Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi, Brigedia Jenerali Julius Gambosi alisema zoezi hilo ni utangulizi wa zoezi kubwa litakalofanyika katika Hifadhi hiyo limekuwa na mafanikio makubwa ambalo limewaongezea uwezo  na ujuzi wapiganaji.

Alisema kuwa lengo la zoezi hilo ilikuwa ni maandalizi ya zoezi kuwa litakalofanyika katika Hifadhi hiyo hivi karibuni ikiwa ni kuwaweka Makanda kuwa tayari wakati wowote kuliinda Tanzania dhidi ya uchokozi wowote.

Brigedia Jenerali Gambosi alisema zoezi hilo lilinakuja litakuwa la kiwango cha juu.

Aidha alisema kuwa eneo hilo ni muhimu kuhakiisha hakuna wavamizi ndani na kuiomba Serikali kuendelea kutoa elimu kwa watu waliomo ndani yake ili waweze kuondoka kwa hiari kwa ajili ya kulitunza na kuendeleza hifadhi kwa matumizi endelevu ambayo yatakuwa na manufaa kwa wananchi wengi.

Alisema kuendelea kuwaacha wavamizi ndani ya Hifadhi hiyo kunaweza kusababisha hata vikundi vya kiharifu kujificha ndani yake.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad