HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 9, 2021

Naibu Spika Tulia Apokea Msaada wa Mabati kutoka Benki ya Maendeleo TIB


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) akifurahi wakati wa makabidhiano ya mabati 324 yaliyotolewa msaada na Benki ya Maendeleo TIB kwa ajili ya kusaidia kuezekea vyumba vya madarasa ya Shule ya Sekondari Itende, mkoani Mbeya.
 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wapili kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Paul Ntinika (kulia), Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Mhe. Dourmohamed Issa (kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Mahusiano ya Kitaasisi wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Patrick Mongella (wapili kulia) wakinyanyua moja ya mabati yaliyotolewa msaada na Benki ya Maendeleo TIB.
 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wapili kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Paul Ntinika (kulia), Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Mhe. Dourmohamed Issa (kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Mahusiano ya Kitaasisi wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Patrick Mongella (wapili kulia) wakijiandaa kunyanyua moja ya mabati yaliyotolewa msaada na Benki ya Maendeleo TIB.
 
Na Mwandishi wetu,  
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini amepokea msaada wa mabati 324 kwa ajili ya kusaidia kuezekea vyumba sita vya madarasa ya Shule ya Sekondari Itende, mkoani Mbeya ambayo haina shule ya sekondari.  
 
Akikabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Mahusiano ya Kitaasisi wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Patrick Mongella alisema benki hiyo imekabidhi msaada huo kwa kutambua nafasi yake kama Taasisi ya Maendeleo, ili kuongeza ustawi wa sekta ya elimu katika Manispaa ya Jiji la Mbeya na Taifa kwa ujumla.    
 
“Kwa kutambua ukweli kuwa suala la elimu ni mojawapo ya maeneo tunayoyaunga mkono tuliona ni vyema Taasisi yetu itoe mchango kwa kuisaidia Manispaa ya Jiji la Mbeya ili kuweza kukamilisha miundombinu ya elimu kwa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza,” alisema Bw. Mongella.  
 
Aliongeza kuwa anaamini msaada huo utachangia malengo ya Serikali ya kuendelea kuboresha elimu inayotolewa ili iweze kutoa maarifa na ujuzi wa kutosha kwa wahitimu katika nyanja zote za elimu hapa nchini.  
 
Kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa makabidhiano hayo alisema kuwa mchango huo unaunga mkono jitihada za Mhe. Rais, Dkt John Pombe Joseph Magufuli za kuendeleza kujenga na kukarabati miundombinu ya elimu ili tunaendelea kuboresha elimu inayotolewa ili iweze kutoa maarifa na ujuzi wa kutosha kwa wahitimu.
 
  Dkt. Tulia aliishukuru Benki ya Maendeleo TIB kwa kusaidia kata ya Itende ambayo haina shule ya sekondari kitu ambacho kinachowalazimu watoto kwenda mbali sana ili kuitafuta elimu hiyo. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad