KAMATI YA BUNGE YA UKIMWI YAFANYA ZIARA MKOA WA NJOMBE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 2, 2021

KAMATI YA BUNGE YA UKIMWI YAFANYA ZIARA MKOA WA NJOMBE  

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Ofisi ya Mkoa wakiongozwa na Mkuu  huo Mhe. Mhandisi Marwa Rubirya. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi wakifuatilia kwa karibu Taarifa ya hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Mkoa wa Njombe ilipofanya ziara yake katika Mkoa wa Njombe hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Godwin Mollel akichangia jambo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi ilipofanya ziara yake katika Mkoa wa Njombe hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Mhandisi Marwa Rubirya akitoa taarifa ya hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Mkoa huo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi ilipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi Mhe. Fatma Tawfiq akifafanua jambo kwenye Kamati hiyo ilipofanya ziara yake katika Mkoa wa Njombe na kupokea Taarifa ya hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Mkoa huo hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)

Na Omary Machunda – Bunge

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi na Dawa za kulevya, imefanya ziara katika Mkoa wa Njombe kuangalia hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Kifua Kikuu (TB) na kuagiza elimu zaidi itolewe kwa jamii ikiwemo matumizi ya mipira ya ya kiume (kondomu) ili kupunguza maambukizi.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa hiyo, Mhe. Fatma Tawfiq, amewataka watendaji wa Mkoa huo waongeze juhudi katika kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na matumizi ya kondomu pamoja na kuhamasisha tohara kwa wanaume.

Naye Naibu Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Godwin Mollel akichangia katika kikao hicho, amemtaka Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Marwa Rubirya kuendesha zoezi la kuzitambua na kuzisaidia Asasi zisizo za Kiserikali (NGOS) zinazoratibu masuala ya Ukimwi ili kufanikisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Awali, akitoa taarifa hiyo ya hali ya maambukizi hayo, kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo, Dkt. Robert Masele ambaye ni mratibu wa Ukimwi Mkoa huo, amesema hali ya maambukizi katika Mkoa imepungua kutoka asilimia 14.8 mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 11.4 mwaka 2017.

Aidha, amesema Halmashauri ya Mji wa Njombe inakadiriwa kuwa na takribani watu 22,537 wanaoishi na Virusi vya Ukimwi idadi ambayo ni kubwa ukilinganisha na Wilaya nyingine zilizomo katika Mkoa huo.

Dkt. Masele ameongeza kuwa pamoja na juhudi zinzofanywa na Serikali ambapo kumekuwa na mpango wa kugawa kondomu kwenye maeneo hatarishi, nyumba za kulala wageni na Ofisim mbalimbali bado hali ya matumizi ya kondomu yako chini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Marwa Rubirya alisema taarifa ya hali ya tohara katika Mkoa huo ilikuwa chini kwa miaka mingi kutokana na tamaduni, mila na desturi za wakazi wa Njombe na hivyo kuongeza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Ameongeza “kwa miaka mingi kumekuwa na tamaduni za kimila zilizopelekea wenyeji wa Mkoa huu kukwepa tohara lakini baada ya Serikali kuanzisha mkakati maalum wa tohara kwa wanaume hali ya maambukizi imekuwa ikishuka kila mwaka”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad