UONGOZI WA BENKI YA EQUITY TANZANIA WATEMBELEA BUNGENI DODOMA LEO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 11, 2021

UONGOZI WA BENKI YA EQUITY TANZANIA WATEMBELEA BUNGENI DODOMA LEO


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (wa pili kulia) akifurahi jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Equity Tanzania, Robet Kiboti (katikati), Mkuu wa Kitengo cha Masoko Benki ya Equity Tanzania, Isabela Maganga (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Benki ya Equity Tanzania, Godwin Semunyu, walipokutana katika viwanja Bunge, jijini Dodoma leo. Kushoto ni Julieth Mahugi, Afisa Mikopo wa Benki ya Equity Tanzania. Uongozi wa Benki ya Equity ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake, leo ulitembelea Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa mualiko wa Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, ikiwa ni katika kudumisha Mahusiano ya Kibiashara baina ya Bunge na Benki hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Equity Tanzania, Robet Kiboti (kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Benki ya Equity Tanzania, Godwin Semunyu (katikati) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi, walipokutana katika viwanja Bunge, jijini Dodoma leo.

Uongozi wa Benki ya Equity Tanzania ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake, Robet Kiboti (wa pili kushoto) ukifatilia vikao vya Bunge jijini Dodoma leo wakiwa ni wageni waalikwa kwa mualiko wa Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai. Wengine pichani ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Benki ya Equity Tanzania, Godwin Semunyu (katikati), Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Isabela Maganga (wa pili kulia), Julieth Mahugi, Afisa Mikopo wa Benki hiyo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad