HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 2, 2021

SERIKALI ITAKAMILISHA UTEKELEZAJI WA VIPAUMBELE VYOTE-MAJALIWA

 


SERIKALI imejipanga vizuri katika kuhakikisha inakamilisha utekelezaji wa vipaumbele vyote ambavyo havikukamilika katika kipindi kilichopita sambamba na kusimamia ipasavyo maeneo mapya yaliyoibuliwa kwenye Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.

 

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo (Jumanne, Februari 2, 2021) Bungeni jijini Dodoma alipowasilisha hoja  kwa ajili ya wabunge kuanza kujadili hotuba ya Rais Dkt. Magufuli aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa bunge la 12 tarehe 13 Novemba 2020.

 

Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kutekeleza na kusimamia masuala muhimu yaliyoelezwa kwenye hotuba ya Rais Dkt. Magufuli ya kuzindua bunge la 11 tarehe 20 Novemba 2015 na amewasisitiza wabunge kutumia vema fursa hiyo adhimu.

 

“Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, sambamba na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020–2025, Serikali imeendelea kusimamia utekelezaji wa ahadi na maelekezo ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa aliyoyatoa wakati akizindua Bunge la 12 sambamba na Bunge la 11.”

 

Amesema Rais Dkt. Magufuli wakati akieleza vipaumbele mbalimbali vinavyotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo, aliweka bayana kuwa mambo yote muhimu yatakayotekelezwa yamebebwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025.

 

“Baada ya hotuba ya Mheshimiwa Rais kutolewa utekelezaji wa maelekezo yake ulianza mara moja kwenye maeneo mbalimbali. Hii ni kutokana na ukweli kwamba Wizara na Taasisi zote za Serikali ziliainisha maeneo ya utekelezaji sambamba na kuja na mipango ya utekelezaji wa muda mfupi, muda wakati na muda mrefu.”

 

“Mheshimiwa Spika, ni ndoto ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kuona Tanzania inajenga uchumi imara, shindani sambamba na kutengeneza ajira za kutosha kwa Watanzania.  Hivyo basi, nitoe rai kwa Waheshimiwa Wabunge wenzangu kutumia vema fursa hii adhimu.”

 

Amesema licha ya kuanza kwa utekelezaji wa masuala mbalimbali yaliyomo kwenye hotuba hiyo, bado michango ya wabunge ni muhimu katika kuisaidia Serikali kutekeleza kikamilifu vipaumbele vilivyoainishwa pamoja na kushughulikia kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad