HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 4, 2021

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUNGUA MAJENGO YA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA PAMOJA NA MIRADI MINGINE YA JESHI HILO MKOANI DODOMA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene wakati akizindua nyumba za makazi ya Maafisa na Askari Magereza katika eneo la Gereza la Isanga Jijini Dodoma leo tarehe 04 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene, Kamishna Jenerali wa Magereza CGP Suleiman Mzee pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu vya Vyombo vya Ulinzi na Usalama, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa nyumba 24 za makazi ya Maafisa na Askari Magereza katika eneo la Gereza la Isanga Jijini  Dodoma leo tarehe 04 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mhandisi Bonanza Marata kuhusu mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha Samani cha Jeshi la Magereza Jijini  Dodoma kabla ya kuweka jiwe la msingi leo tarehe 04 Januari 2021 katika eneo la Msalato.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene wakati  akiweka jiwe la Msingi ujenzi wa Kiwanda cha Samani cha Jeshi la Magereza Msalato Jijini Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua na Kuendesha magari mapya ya Jeshi la Magereza nchini mara baada ya kufungua Majengo ya Makao Makuu ya Jeshi hilo Msalato Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Maafisa na Askari Magereza mara baada ya kufungua Majengo ya Makao Makuu ya Jeshi hilo Msalato Jijini Dodoma. 


Taswira ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza yaliyopo Msalato Jijini Dodoma.( PICHA NA IKULU.) 

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad