KAMPUNI ya Michezo ya kubashiri Nchini MERIDIAN BET imejitokeza na kusaidia kiasi cha shilingi Millioni Moja kwa mtoto Rehema Faustine (1) aliyezaliwa na Kansa ya Macho hali iliyopelekea kushindwa kuona wala kusikia huku baba yake akimtelekeza mtoto huyo kutokana na matatizo aliyonayo.
Awali akisimulia mama mzazi wa mtoto huyo Nadia Faustine (24) amesema amebahatika kupata mtoto mmoja aitwaye Rehema ambaye amezaliwa na Ulemavu wa macho (KIPOFU) baada ya kupata kansa ya macho akiwa tumboni.
Akisimulia kwa uchungu Nadia anasema alipata ujauzito na baada ya miezi 4 akaambiwa anawatoto mapacha tumboni lakini mmoja amefariki mmoja mzima hivyo akaambiwa asubilie hadi miezi sita ili yule mzima akue hali iliyopelekea matatizo makubwa kwa mtoto aliyekuwa hai
Akizungumza wakati akitoa msaada kiasi cha Shilingi Millioni 1, Meneja Ustawi Meridian Bet Amani Maeda amesema wameguswa na matatizo anayoyapitia mtoto huyo hivyo wakaguswa kumsaidia ili aweze kupata matibabu zaidi
Naye Mkuu wa Utawala Meridian Bet, Cornelius Bornman amesema Kampuni hiyo imekuwa ikishiriki katika matukio mbalimbali ya kijamii kwa lengo la kusaidi jamii zenye uhitaji huku akionyesha kusikitishwa na matatizo ya mtoto huyo
Kwa Upande wake Nadia Faustine ameishukuru kampuni ya Meridian Bet kwa kumsaidia mtoto wake fedha kwa ajili ya matibabu kwani anapitia katika wakati mgumu kutokana na matatizo aliyonayo
Kwa sasa mtoto huyo anatakiwa kufanyiwa Operation ili kutolewa mabaki ya macho yaliyosalia ili yasimsababishie matatizo kwenye mishipa ya fahamu ambapo gharama yake ni kiasi cha shilingi 1, 500, 000 ( Milioni moja na laki tano).
No comments:
Post a Comment