HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 16, 2021

CDF MABEYO ASISITIZA USHIRIKANO KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo ( wa sita wa mbele kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( wa tano kutoka kulia)leo alipofika kwa ajili ya ziara ya kikazi. Na Tiganya Vincent RS Tabora

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo amevitaka vyombo vya ulinzi wa usalama kuendeleza mshikamano na ushirikiano uliopo ambao umesaidia kujenga imani kubwa kwa wananchi na kuimarisha ulinzi wa Nchi.

Alisema panapo kuwemo na mshikamano wananchi wanaona na wanakuwa na imani kubwa kwao na kuwaunga mkono.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania Jenerali Mabeyo alisema hayo leo alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora akiwa ziarani mkoani humo.

Alisema katika hali iliyopo ya sasa ulimwenguni vyombo vya ulinzi na usalama vinatakiwa kuwa na ushirikiano kwa ajili ya kukabiliana na mtu yoyote toka ndani na nje mwenye nia mbaya.

“Adui wa sasa anaweza asijitokeze mmoja kwa mmoja , bali anaweza kuwa miongoni mwenu…hivyo ushirikiano wa vyombo vya ulinzi na usalama ni jambo muhimu katika kuendelea kudumisha amani na utulivu nchini”alisisitiza.

Jenerali Mabeyo aliwataka vyombo vya Ulinzi na Usalama waliopo katika ngazi za chini kuendelea kuimarisha ushirikiano kama wanavyofanya kwa ngazi ya Kitaifa.

Alisema kwa ngazi ya Taifa kila wakati wanashirikiana na wapo pamoja katika utekelezaji wa majukumu yao.

Aidha Jenerali Mabeyo amewashukuru wananchi wa Tanzania kwa utulivu wa hali ya juu waliouonyesha wakati zoezi la uchaguzi Mkuu uliopita.

Alisema hali ilitokana imani kubwa ambayo wananchi wanayo kwa vyombo vyao vya ulinzi na usalama katika kulinda amani na usalama wa Nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati alisema wameanzisha utaratibu wa kukutana kila mwisho mwezi kwa vyombo vote vya ulinzi na usalama mkoani humo kwa lengo la kujenga umoja.

Alisema kuwa katika kufakikisha hilo wanafanya mazoezi ya pamoja na kujadiliana ikiwa ni sehemu kuwa kitu kimoja.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo (kulia) akisaini vitabu wa wageni leo katika ziara yake ya kikazi mkoani Tabora. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati(katikati) akitoa taarifa leo ya hali ya ulinzi na usalama kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo(kulia) aliyefika kwa ajili ya kusaini vitabu vya wageni akiwa ziarani mkoani humo.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) akiagana na Mkuu wa |Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati (kulia) leo mara baada ya kusaini vitabu vya wageni akiwa katika ziara ya kikao katika Mkoa huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad