Mwandishi wetu
KAMPUNI ya kubashiri matokeo ya Meridian Bet imepanua wigo katika kusaidia jamii na jana imesaidia kufanikisha mafunzo ya lishe kwa wakazi wa Mbezi Juu, Dar es Salaam.
Meridian Bet ambayo mbali na kuwa kampuni ya michezo ya kubashiriki matokeo imekuwa ikijitoa kusaidia jamii yenye uhitaji katika nyanja tofauti.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyoongozwa na Afisa Lishe wa manispaa ya Kinondoni, Janeth Mzava na diwani wa Mbezi Juu, Anna Lukindo, Meneja Ustawi wa Meridian Bet, Amani Maeda alisema wamesaidia mafunzo hayo ili jamii ipate kuelewa umuhimu wa lishe bora.
"Lishe ni muhimu sana katika maisha yetu, unapokula mlo kamili hata kupata magonjwa ni kwa kiasi kidogo, mfano sasa dunia ina tunachangamoto ya corona.
"Hivyo tunapokula lishe bora kwa kuzingatia misingi ya mlo kamili, miili yetu inakuwa imara," alisema Amani.
Alisema kampuni ya Meridian Bet kusaidia mafunzo hayo ambayo yamekuwa na mtizamo chanya kwa jamii ya eneo la Mbezi Juu.
Diwani wa eneo hilo, Anna Lukindo aliishukuru Meridian Bet kwa msaada huo na kueleza kwamba mafunzo hayo yamewasaidia kina mama wengi na hata baadhi ya kina baba wa eneo hilo.
"Wamejifunza mlo kamili unapaswa uweje? njia ya kumhudumia mtoto katika siku 1000 za mwanzo, lishe kwa mtu anayetakiwa kupunguza uzito na mambo mbalimbali ya afya," alisema.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Stumai Rajabu alisema mafunzo hayo yamemfundisha umuhimu wa lishe bora.
"Mwanzo mwanangu nilikuwa nampa ugali na mchuzi na maji, lakini baada ya mafunzo nimeelimika kwamba ili mtoto akue vizuri anahitaji mchanganyiko wa makundi yote matano ya vyakula, nitaanza kuzingatia hilo," alisema.
Hongereni meridian
ReplyDeleteSafi sana meridianbet
ReplyDeleteGud
ReplyDelete