Makamu wa rais wa Zanzibar Maalim Seif afariki dunia - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 17, 2021

Makamu wa rais wa Zanzibar Maalim Seif afariki dunia


 

 Makamu wa Kwanza wa Rais visiwani Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amefariki dunia. Habari hizo zimethibitishwa leo na Rais wa Zanzibar, Dokta Hussein Ali Mwinyi wakati akizungumza na waandishi wa habari visiwani humo.

Akitowa tangazo la kifo hicho mchana huu, Rais Mwinyi amesema makamu wake huyo wa kwanza amefariki dunia saa tano asubuhi ya leo wakati akitibiwa jijini Dar es Salaam. Bila ya kutaja ugonjwa uliokuwa ukimsibu, rais huyo ametowa mkono wa pole kwa Wazanzibari na Watanzania wote.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amesema ameshtushwa na kifo cha Maalim Seif. Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Rais Mwinyi, familia ya Seif, Wazanzibari, wnachama wa ACT-Wazalendo pamoja na Watanzania wote kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad