Benki ya NMB imekabidhi mabati
200 na vifaa vyengine vya ujenzi kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya
madarasa ya Shule ya Sekondari ya Jambiani, Kusini Unguja. Akizungumza
katika hafla ya makabidhianao hayo iliyofanyika skulini hapo, Meneja wa
NMB Kanda ya Dar-es-salam, Donatus Richard alisema wameamua kutoa msaada
huo ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika
kuimarisha sekta ya elimu.
“Benki ya NMB tumeamua kushirikiana
pamoja na Jamii yote inayozunguka eneo la Jambiani kuchangia mabati 200
kwa ajili ya kutatua changamoto ya kuvuja kwa madarasa wakati wa mvua”
alisema Donartus.
Aliongeza kuwa elimu ni kichocheo cha maendeleo
hivyo kuna kila sababu kwa watoto kupata mazingira mazuri ya kupata
elimu na kusisitiza ndio maana benki ya NMB imeamua kuisaidia skuli
hiyo.
Nae Mwakilishi wa Jimbo la Paje ambae pia ni Waziri wa
Kilimo, uvuvi, mifugo na umwagiliaji, Sudi Nahoda ameishukuru benki hiyo
kwa msaada huo na kusema utasaidia kutatua changamoto ya kuvuja kwa
skuli hiyo.
“Nikuhakikishieni kuwa msaada huu mliotupatia una
thamani kubwa na kiuhalisia NMB ni moja kati ya mashirika yanayojali
Jamii katika kuleta maendeleo.” Alisema Mhe. Sudi
Kwa upande wake
kaimu mwalimu mkuu wa Skuli ya Jambiani, Haji Haji ameishukuru NMB kwa
msaasa huo, amesema kwa muda sasa wamekuwa wakikabiliwa na ubovu wa
madarasa ambapo wanafunzi wamekuwa wakishindwa kuhudhuria masomo katika
vipindi vya mvua.Meneja
wa NMB Kanda ya Dar es salaam, Donatus Richard (mwenye suti wapili
kulia) akipeana mkono na Waziri wa Kilimo Maliasili na Umwagiliaji
Zanzibar, Soud Nahoda Hassan wakati wa makabidhiano ya vifaa vya ujenzi
vikiwemo mabati mia mbili kutoka Benki ya NMB kwa ajili ya shule ya
Jambiani Sekondari. Kushoto ni Meneja Tawi la NMB Tawi la Zanzibar,
Abdalla Duchi
Meneja
wa NMB Kanda ya Dar es salaam, Donatus Richard, Waziri wa Kilimo
Maliasili na Umwagiliaji Zanzibar, Soud Nahoda Hassan wakifurahia pamoja
na Walimu, Wanafunzi na Wazazi baada ya Makabidhiano ya mabati 200 na
vifaa vyengine vya ujenzi kwa ajili ya shule ya Jambiani Sekondari.
Meneja
wa NMB Kanda ya Dar es salaam, Donatus Richard, Waziri wa Kilimo
Maliasili na Umwagiliaji Zanzibar, Soud Nahoda Hassan pamoja na baadhi
ya wazazi waliohudhuria hafla na makabidhiano ya mabati 200 na vifaa
vyengine vya ujenzi kwa ajili ya shule ya Jambiani Sekondari.
Saturday, February 20, 2021

Home
ELIMU
BENKI YA NMB YAKABIDHI MABATI 200 NA VIFAA VINGINE VYA UJENZI KUKARABATI VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA SEKONDARI JAMBIANI KUSINI UNGUJA.
BENKI YA NMB YAKABIDHI MABATI 200 NA VIFAA VINGINE VYA UJENZI KUKARABATI VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA SEKONDARI JAMBIANI KUSINI UNGUJA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment