HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 13, 2021

WALIOSHINDA SHINDANO LA CSI KUWAWEZESHA VIJANA KUTIMIZA NDOTO ZAO WAANZA MASOMO CHUO CHA MAZNAT


Meneja wa Programu za Vijana katika shirika la Childbirth Survival International(CSI) Ester Mpanda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwakabidhi kwa walimu vijana wawili  hao wawili ambao wamewapata ufadhili wa masomo kutoka CSI katika Chuo cha Urembo Maznat kilichopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam leo.
Suzana Kanyara ambaye alipata ufadhili wa Masomo ya Urembo kutoka shirika la Childbirth Survival International(CSI)  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna alivyojipanga mara baada ya kupata fursa ya kupata mafunzo ya Chuo cha Urembo Maznat kilichopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam leo.
David Francis ambaye alipata ufadhili wa Masomo ya Urembo kutoka shirika la Childbirth Survival International(CSI)  akizungumza na waandishi wa habari pamoja na kushukuru shirika hilo kwa kumpatia nafasi hiyo ili kujiendeleza kwenye fani ya urembo kupitia Chuo cha Urembo Maznat kilichopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam leo.
Mwalimu wa Chuo cha Urembo Maznat, Juma Kimwaga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna walivyowapokea wanafunzi hao na kutoa shukrani kwa shirika la Childbirth Survival International(CSI) kuendelea kuwasaidia vijana ili kufikia malengo yao.
Meneja wa Programu za Vijana katika shirika la Childbirth Survival International(CSI) Ester Mpanda pamoja na wanafunzi wakipata maelekezo kutoka kwa uongozi wa Chuo cha Urembo Maznat mara baaada ya kuwasili chuoni hapo kwa ajili ya kuanza masomo ya urembo.
 
Na Said Mwishehe, Michuzi TV 
SHIRIKA la Childbirth Survival International(CSI)ambalo imejikita katika kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua limewashauri vijana kuhakikisha wanachangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza ili kufanikisha ndoto zao kimaisha na kuweza kujitegemea kiuchumi.
CSI imesema pamoja na mkakati wake wa kuendelea kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Serikali katika kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua na wale walio chini ya miaka mitano, bado inao wajibu wa kuhakikisha ndoto za vijana wa kitanzania zinatimia , hivyo wameamua kutoa ufadhili wa masomo kwa vijana wawili katika Chuo cha Urembo cha Maznat baada ya kuwapata kupitia shindano maalum ambalo lilifanyika mwzi mmoja uliopita.
Hayo yamesemwa leo na Meneja wa Programu za Vijana kutoka CSI Ester Mpanda baada ya kuwakabidhi kwa walimu vijana wawili ambao wamewapatia ufadhili wa masomo katika Chuo hicho cha Urembo. Akizungumza leo Januri 13,2021 jijini Dar es Salaam Meneja wa Programu za Vijana kutoka CSI Ester Mpanda amesema wanayo fufaraha kubwa kwani vijana hao wanakwenda kutimiza ndoto zao za kujitegemea kiuchumi na kimaisha pindi watakapohitimu masomo yao.
Akifafanua zaidi Ester Mpanda amesema shirika hilo ambalo limeanzishwa na mama wawili ambao ni Stella Mpanda anayeishi nchini Tanzania na Tausi Kagasheki anayeishi Marekani mbali ya kujikita katika kupunguza vifo vya mama na mtoto, wameona kuna kila sababu sasa ya kuhakikisha linatoa ufadhili wa masomo kwa vijana wa kitanzania ili waweze kutimiza ndoto zao ikiwa pamoja na kujiinua kiuchumi baada ya kuhitimu masomo ya urembo katika chuo hicho.
"Chuo hiki kinafundisha masuala ya urembo, upambaji, kusuka, kupamba maharusi, hivyo vijana hawa ambao leo hii wameanza masomo yao hapa baada ya kuendesha shindano la kutafuta vijana ambao wanatamani kutimiza ndoto zao kimaisha.
"Tunachoweza kueleza CSI tumeamua kutoishia kwenye kupunguza vifo vya mama na mtoto, bali tunayo nafasi ya kujenga maisha ya vijana wa kitanzania ambao tunatarajiwa wawe baba au mama wa kesho, tunaka kujenga  vijana watakaokuwa baba na mama bora huko baadae ambao watakuwa na uchumi unaowezesha kuendesha familia zao bila matatizo yoyote,"amesema Mpanda.
Amesisitiza masomo ambayo vijana hao wameyaanza leo katika chuo hicho yatachukua muda wa miezi mitatatu  na baada ya hapo wataanza kujitegemea katika safari yao ya kimaisha."Nawashukuru Chuo cha Maznat kwa kukubali kufanya kazi na sisi na kukubali kutupa nafasi ya kuja hapa na kuwaleta vijana hawa ambao kwa upande wetu tutagharamia kila kitu kinachohusu masomo yao kwa muda wote.
"Ninachoweza kuwaambia vijana mkisikia fursa tunaomba mzichangamkie kwani huwezi jua,hawa vijana ambao wanaanza masomo leo walikuja tu kwenye shindano letu na wala hawakujua kama watashinda lakini walipata nafasi na leo wako hapa..Nafasi ziko nyingi hivyo ni jukumu la vijana kuzitafuta kokote ziliko."
Kuhusu changamoto ya kuchagua kazi, Mpanda amesema ni kweli kuna baadhi ya vijana wamekuwa na utamaduni wa kuchagua kazi, jambo linalochangia kuwakwamisha kimaendeleo, hivyo ni vema wakabadilika.
"Kwa sasa kuna utofauti kidogo vijana wamebadilika wameanza kushughulika katika kazi mbalimbali maana wameona hali ilivyo na wamekubali matokeo, wanafanya kazi yoyote ilimradi iwe ya halali na isiyovunja sheria."
Kwa upande wake mmoja ya walimu katika  Chuo cha Urembo Maznat Juma Kimwaga amesema wamefurahi kuwapokea wanafunzi hao wawili akiwemo wa kijana wa kiume."Viajana wengi wa kiume huwa wanachagua kazi na hasa hizi za urembo lakini ukweli kazi ya urembo ina fursa ila hawajui hilo.
"Tunawapongeza CSI kwa uamuzi huu mzuri wa kufanikisha ndoto za vijana hao kwa kuwaleta katika chuo chetu, tunaamini wakitoka hapa watakwenda kujitegemea kimaisha,"amesema.
Aidha amesema katika fani ya urembo, kuna changamoto kubwa ya kupata wanaume wakiamini sio kazi ambayo wanastahili kuifanya, hivyo kupata kijana wa kiume kwani ni jambo la kujivunia."Vijana hawana sababu ya kuigopa tasnia hii ya urembo, sisi tuko huku maisha yanakwenda na maendeleo tunafanya kwa kiwango kikubwa tu."
Kwa upande wa vijana hao ambao ni Susan Kanyara na David Frank wamesema wanashukuru kwa kupata fursa hiyo ya kudhaminiwa na CSI kusoma chuoni hapo.Waliipata nafasi hiyo baada ya kushinda shindano la CSI lililofanyika mwezi mmoja uliopita. 
Susan Kanyara amesema leo wameanza masomo katika chuo hicho na ni matumaini yake anakwenda kutimiza ndoto zake za kimaisha na hasa kujitegemea.
Wakati David Francis amesema nafasi hiyo aliyoipata ni ya kipekee, hivyo atasoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zake huku akitoa shukrani kwa CSI kwa hatua ambayo wameichukua ya kusaidia vijana walioko mtaani kutimiza ndoto zao kupitia ufadhili huo wa masomo.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad