Fundi sanifu wa moyo
(Cardiovascular technologist) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Paschal
Kondi akimpima mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography –
ECG) mchezaji wa
timu ya taifa chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes Kimwe Kisare wakati timu hiyo
ilivyofika JKCI kwa ajili ya kuwafanyiwa uchunguzi wa afya ya moyo kabla ya
kushiriki mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika
nchini Mauritania mwezi Februari mwaka huu.
WACHEZAJI 30 wa timu ya Taifa chini ya miaka 20
Ngorongoro Heroes wamefanyiwa uchuguzi wa kina wa magonjwa ya moyo kama Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) linavyoelekeza kabla ya kuanza kwa mashindano ya
kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ni lazima wachezaji wanaoshiriki mashindano
hayo wapimwe afya zao.
Vipimo walivyofanyiwa wachezaji hao ni vya kuangalia
jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph), mfumo wa umeme wa moyo
unavyofanya kazi (Electrocardiography –ECG), na vipimo mbalimbali vya damu
kuangalia afya ya mwili kwa ujumla. Upimaji huu umefanywa na madaktari bingwa
wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI.)
Vipimo vya damu vilivyofanywa kwa wachezaji hao ni
pamoja na kuangalia kama kuna maambukizi yoyote kwenye damu, kipimo cha
kuangalia viwango vya mafuta katika mwili, kuchunguza madini ya chumvi mwilini
na kipimo cha kuangalia kiwango cha sukari mwilini.
Matokeo ya vipimo hivyo yatasaidia kufahamu afya za
wachezaji na utimamu wao wa kimwili kabla ya kwenda kushiriki katika mashindano
ya AFCON yanayotarajia kuanza tarehe 14/02/2021 huko nchini Mauritania.
Tunatoa wito kwa vilabu vya mpira hapa nchini
kuwaleta wachezaji wao kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo hii
itawasaidia wachezaji hao kufahamu kama wanamatatizo au la na kuepukana na vifo
vya ghafla vinavyoweza kuwapata wakiwa uwanjani. Kwa upande wa wananchi kabla
ya kujiunga na vilabu vya mazoezi ni muhimu wakapima afya zao yakiwemo magonjwa
ya moyo..
No comments:
Post a Comment