NA Neema Mbuja, Rukwa
Shirika
la umeme Tanzania TANESCO kupitia Idara ya masoko imeendelea na kampeni
ya kutoa Elimu kwa wamiliki wa viwanda,machimbo ya madini, na mashine
za kusaga kwa mkoa wa Rukwa ili kuwapatia Elimu juu ya matumizi Bora ya
umeme sanjari na kukagua miundo mbinu ya umeme pamoja na mota
zinazotumiwa kwenye kuendesha mashine viwandani
Miongoni
mwa Elimu wanayopatiwa Ni pamoja na namna ya kutumia vifaa ambavyo
vinatumia umeme kidogo, umuhimu wa kukagua mota zao Mara kwa Mara kwa
ajili ya kuleta ufanisi na Usalama wa miundo mbinu ya TANESCO kwenye
maeneo yao
Akizungumza
na wamiliki wa viwanda kwenye Wilaya za Sumbawanga mjini na Laela ,
mhandisi kutoka kutoka idara ya utafiti Baraka Kanyika amesema kuwa
kwa Sasa baadhi ya viwanda vinatambua umuhimu wa kufunga power factor
ingawa baadhi bado hawajatambua
Kuhusu
wamiliki wa mashine za kusaga Kijiji Cha muze Wilaya ya Laela mkoa wa
Rukwa mhandisi Kanyika ameshauri kuendelea kuwapatia Elimu ya umuhimu wa
kukagua mota zinazoendesha mashine zao Mara kwa Mara ili kuziongezea
ufanisi wa utendaji kàzi na kulinda miundo mbinu ya shirika.
<
No comments:
Post a Comment