Mgeni rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Abdul Maulid pamoja na Mwanamitindo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Flaviana Matata akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi,
walimu, maafisa elimu wa wilaya zote za Dar es Salaam pamoja na wadau
mbalimbali wa masuala ya mtoto wa kike mara baada ya kufanyika kwa
uzinduzi wa ufadhili
wa elimu kwa wasichana 1000 kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na
kati yao wasichana 250 wanatoka Mkoa wa Dar es Salaam ambao pia
watapata taulo za kike za Lavy bure kila mwezi kwa kipindi cha mwaka
mmoja kwa kuanzia.
Katika
jitihada za kuendelea kuisaidia jamii hasa mtoto wa kike Mwanamitindo
na Mjasiriamali Flaviana Matata chini ya taasisi yake ya ‘Flaviana
Matata Foundation’ ambayo ilianzishwa kwa lengo la kusomesha watoto wa
kike watokao kwenye mazingira magumu pamoja na kuhamasisha upatikanaji
wa elimu bora katika mazingira rafiki na salama kwa wanafunzi kupitia
utoaji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia, ujenzi na ukarabati wa
vyoo, madarasa, ofisi na nyumba za walimu.
Leo
Flaviana amezindua rasmi ufadhili wa elimu kwa wasichana 1000 kutoka
sehemu mbalimbali za Tanzania na kati yao wasichana 250 wanatoka Mkoa wa
Dar es Salaam ambao pia watapata taulo za kike za Lavy bure kila mwezi
kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa kuanzia. Msaada huu umelenga
kuhakikisha hedhi kutokua kikwazo kwa watoto wa kike wa Kitanzania
kupata elimu bora itakayoweza kuwajengea misingi imara ili waweze
kuzifikia ndoto zao kupitia.
Ufadhili
huu umepatikana baada ya kuchangisha pesa kupitia kampeni ya ‘Donate A
Period’ iliyofanywa na Flaviana pamoja na baadhi ya marafiki zake nchini
Marekani kwa lengo la kuhakikisha watoto wa kike hawakosi masomo
kwasababu ya kutomudu gharama za taulo za kike(Sanitary Pads).
Akiongea
na wana habari Flaviana amesema “Kuna watoto wengi hasa wakike ambao
wapo kwenye mazingira magumu na wanakosa haki yao ya msingi ya kupata
elimu bora kutokana na changamoto walizonazo. Hivyo nafurahi sana
tumeweza kufanikisha ufadhili huu kwa mabinti 1000 ambao kwa namna moja
au nyingine ufadhili huu utaenda kubadilisha maisha yao hasa wakiwa
shuleni”
Flaviana
ameongeza pia “Natamani ufadhili huu uwe ni mwanzo tu wa kuhamasisha na
kushawishi serikali, makampuni binafsi na jamii kwa ujumla kuunga mkono
juhudi hizi ili kupitia Flaviana Matata Foundation tuweze kuwafikia na
kuwasaidia watu wengi zaidi wenye uhitaji ambayo hii itasaidia pia
kuinua jamii zetu na nchi yetu kwa ujumla”
“Inapendeza
sana kuona juhudi mbalimbali zinazofanywa na watu binafsi katika
kuboresha maisha ya watanzania hasa kwenye upande wa Elimu na kwa watoto
wakike. Itapendeza sana kama watu mbalimbali wakijitokeza kusaidia
juhudi hizi zifike mbele zaidi kwa chochote kile au vyovyote vile
tujaribu kushiriki kwenye kuwainua mabinti lakini kuinua nchi yetu
ambayo inahitaji kila mtu kuwajibika ili iende mbele” aliongea mgeni
rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Abdul Maulid aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge.
Kipekee
kabisa Flaviana Matata anawashukuru marafiki zake waliochangia kwenye
kampeni hii ya ‘Donate A Period’ kwa kufanikisha hili, Mkuu wa mkoa kwa
kukubali kuwa mgeni rasmi, wakuu wa wilaya , wakurugenzi, maafisa elimu
na watu wote waliofanikisha shughuli hii.
Afisa
Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Abdul Maulid akizungumza na
wanafunzi, walimu na maafisa elimu wa wilaya zote za Dar es Salaam
wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi
wa ufadhili wa elimu kwa wasichana 1000 kutoka sehemu mbalimbali za
Tanzania na kati yao wasichana 250 wanatoka Mkoa wa Dar es Salaam ambao
pia watapata taulo za kike za Lavy bure kila mwezi kwa kipindi cha
mwaka mmoja kwa kuanzia. Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Abdul Maulid alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Abubakar Kunenge.
Mwanamitindo
na Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Flaviana Matata
akizungumza na wanafunzi, walimu na maafisa elimu wa wilaya zote za Dar
es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi
wa ufadhili wa elimu kwa wasichana 1000 kutoka sehemu mbalimbali za
Tanzania na kati yao wasichana 250 wanatoka Mkoa wa Dar es Salaam ambao
pia watapata taulo za kike za Lavy bure kila mwezi kwa kipindi cha
mwaka mmoja kwa kuanzia.
Baadhi
ya wanafunzi, walimu, maafisa elimu wa wilaya zote za Dar es Salaam
pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya mtoto wa kike wakifuatilia
hotuba ya Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Abdul Maulid alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Abubakar Kunenge wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi
wa ufadhili wa elimu kwa wasichana 1000 kutoka sehemu mbalimbali za
Tanzania na kati yao wasichana 250 wanatoka Mkoa wa Dar es Salaam ambao
pia watapata taulo za kike za Lavy bure kila mwezi kwa kipindi cha
mwaka mmoja kwa kuanzia.
Mwanamitindo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Flaviana Matata akikabidhi taulo za kike za Lavy kwa Afisa
Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Abdul Maulid zitakazokuwa
zinatolewa kila mwezi kwa kipindi cha mwaka mzima katika shule zilizopo
jijini Dar es Salaam. Mwanamitindo
na Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Flaviana Matata akiwa
kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali
zilizopo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi
wa ufadhili wa elimu kwa wasichana 1000 kutoka sehemu mbalimbali za
Tanzania na kati yao wasichana 250 wanatoka Mkoa wa Dar es Salaam ambao
pia watapata taulo za kike za Lavy bure kila mwezi kwa kipindi cha
mwaka mmoja kwa kuanzia.
No comments:
Post a Comment