RC KUNENGE AKUTANA NA WAZEE WA MKOA WA DAR ES SALAAM, AWAAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZAO. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 8, 2021

RC KUNENGE AKUTANA NA WAZEE WA MKOA WA DAR ES SALAAM, AWAAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZAO.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge leo amekutana na kufanya kikao na Wawakilishi wa Wazee wa Mkoa huo kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili Wazee ili Serikali iweze kuzifanyia kazi.

Katika kikao hicho RC Kunenge amepokea changamoto na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa Wazee hao ambapo zipo changamoto zililizopatiwa majibu ya papo kwa papo na nyingine za kisera na kisheria ambazo ameahidi kuzifikisha katika ngazi husika.

Aidha RC Kunenge amewashukuru na kuwapongeza Wazee wote wa Mkoa huo kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya Katika kueneza Busara, hekima na maarifa kwa jamii Jambo linalosaidia kuwa na kizazi kinachofuata maadili na kulinda amani na usalama mkoani humo.

Hata hivyo RC Kunenge amewaeleza Wazee hao kuwa ofisi yake iko wazi kupokea na kusikiliza ushauri kutoka kwa Wazee na ataweka utaratibu kukutana na Wazee wa Mkoa huo kila baada ya miezi mitatu.

Pamoja na hayo RC Kunenge amewasihi Wazee kuendelea kuwa kisima Cha maarifa na kuhakikisha wanakuwa washauri wazuri wa Amani, Upendo, upatanisho na watoe nasaha kwa jamii.

Kwa upande wao Wazee walioshiriki kikao hicho wamemshukuru RC Kunenge kwa namna anavyowakumbuka na kuwathamini Wazee wa Mkoa huo na wamemuahidi watampatia ushirikiano wa kimawazo Katika kila Jambo.

WAZEE NI HAZINA, PALIPO NA WAZEE HAKUNA KINACHOHARIBIKA. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad