HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 7, 2021

POLISI WANNE WATIMULIWA KAZI KWA UTOVU WA NIDHAMU ARUSHA

 


Na Woinde Shizza, ARUSHA

JESHI la Polisi nchini limewafukuza kazi  askari wake wanne
kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu  ikiwemo rushwa na wizi.

Akiongea na vyombo vya habari Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Salumu
Hamduni alisema kuwa askari hao wametimuliwa kazi jana, januari 6.

Alisema kabla ya kufukuzwa  kazi kwa askari hao, walifikishwa kwenye
mahakama ya kijeshi na kukutwa na hatia na kwamba watafikishwa
mahakamani kama vibaka wengine wanaojihusisha na matukio ya uhalifu.

"Askari hao tumewafukuza kazi baada ya kuwafikisha kwenye mahakama ya
kijeshi na watashtakiwa kama vibaka wengine wa kawaida."alisema Kamanda

Aliwataja askari hao kuwa ni pamoja na  askari mwenye namba G. 5134 DC
Heavenlight Mushi  aliyekuwa Askari kitengo cha Intelijensia Mkoa wa
kipolisi kinondoni jijini Dar es Salaam, H.125 PC Gasper Paul kitengo
cha Intelijensia makao makuu Dodoma na H.1021 PC Bryton Murumbe
aliyekuwa askari wa kawaida mkoani Dodoma.

Kamanda alifafanua kwamba askari hao wamefukuzwa kazi kutokana kwa
kosa la kumteka mfanyabiashara wa Madini jijini Arusha, Sammy Mollel
ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya madini ya Germs and Rocks Venture
ya jiji Arusha na kujipatia kiasi cha sh, milioni 10 kinyume cha
sheria.

Alisema askari hao wakikamatwa desemba 24, 2020 katika ofisi za
mfanyabiashara huyo baada ya kufika kwa ajili ya kuchukua mgao wa pili
wa shilingi milioni 20 kati ya milioni 30 walizohitaji na kupatiwa
sh,milioni 10.

Mwingine aliyefukuzwa kazi ni askari mwenye namba F.1445 CPL Koplo
William Joseph mkazi wa Muriet jiji Arusha ambaye alikamatwa jana
nyumbani kwake akiwa na na bidhaa mbalimbali haramu ikiwemo misokoto
ya bangi.

Alisema kuwa askari huyo alikutwa na misokoto 20 ya bangi 
kwenye gari lake,kujiunganishia umeme wa wizi kinyume cha
sheria, kupatikana na pombe ya gongo lita tano na lita mafuta ya Dizel
Lita 85.

Pia alikutwa na vyuma vya bomba kinyume na taratibu, pombe ya viroba
boksi 84 iliyookatazwa na serikali,chupa 9 za konyagi na pakti 3 za
pombe aina ya kiroba .

Kamanda alisema kuwa upelelezi wa matukio hayo umekamilika na majalada
yamepelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa ajili ya hatua zaidi na
majalada hayo yakirudi watafikishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad