HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 18, 2021

NAIBU WAZIRI BASHE AWAHAMASISHA VIONGOZI WA MKOA WA SIMIYU KUANZISHA MASHAMBA MAKUBWA

 

Naibu Waziri Kilimo Hussein Bashe akiwa amebeba dumu la lita 5 la mafuta ya alizeti alilopewa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka baada ya kutembelea kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti cha Bugali Investment Ltd cha mkoani Simiyu mara baada ya Naibu Waziri Bashe kutembelea kiwanda hicho cha kukamua mafuta ya alizeti kwa kiwango cha hali ya juu (Double refined).

NAIBU Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (Jana) tarehe 17 Januari, 2021 amewasili mkoa wa Simiyu kwa ajili ya tukio la tukio la kihistoria la utiaji saini mkataba wa kuongeza tija na uzalishaji katika zao la pamba kati ya Bodi ya Pamba, Vyama vya Ushirika na Vyama vya Msingi vya Mazao (AMCOS) na Tume ya Maendeleo ya Ushirika na kuwahamasisha Viongozi wa mkoa wa Simiyu kuanzisha mashamba makubwa (Block Farming) ya kilimo cha alizeti.

Waziri Bashe amesema Wizara ya Kilimo imedhamiria kutekeleza kauli ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati akizindua Bunge la 13 na kusisitiza umuhimu wa kuitumia Sekta ya Kilimo mazao kuleta maendeleo ya kweli kwa Watanzania na kuwafanya Watanzania kuwa mabilionea.

Waziri Bashe amewaaambia Viongozi wa mkoa wa Simiyu kuwa ili mkoa uwe na uwekezaji unaolipa ni lazima kufikiria kutumia uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa njia ya uwekezaji katika mashamba makubwa (Block Farming) ambapo Naibu Waziri Bashe ameahidi Wizara itatoa Wataalam kuanzia kwenye kufanya uchunguzi wa udongo kabla ya kuanza kwa uzalishaji na baadae utaalam katika kilimo cha zao la alizeti.

Waziri Bashe amesema mkoa wa Simiyu utapaa kimapato kutokana na uanzishwaji wa mashamba makubwa (Block Farming) kwa kuwa ni rahisi kuendesha mashamba makubwa ambapo ni rahisi kuwasaidia Wakulima wakiwa katika eneo moja lakini pia ni rahisi kutoa utaalam na ushauri wa kuandaa mashamba, utoaji wa pembejeo bora, usimamizi.

“Ni rahisi kuwapa mikopo na teknolojia za kilimo na uvunaji kwa Wakulima walio pamoja kuliko walio mbali.”

“Ni rahisi kutumia teknolojia za uvunaji pamoja na uhifadhi lakini pia kazi uwa ni rahisi kwa mnunuzi anapotaka kununua mzigo na kuuchukua kutoka kwa Wakulima walio katika eneo moja.”

“Naomba pia niwaeleze ni rahisi pia Halmashauri zenu kukusanya tozo na ushuru mbalimbali kwa Wakulima walio kwenye shamba la pamoja.” Amekaririwa Naibu Waziri Bashe.

Waziri Bashe ameongeza kuwa Sekta ya Kilimo mazao hususan kilimo cha alizeti; Ikitumika ipasavyo mkoa wa Simiyu unaweza kuongeza mapato ukilinganisha na Sekta nyingine za kiuchumia.

“Napenda niwakikishie kuwa soko la alizeti lipo wazi na mnafahamu kuwa Serikali inatumia zaidi ya Bilioni 443 kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi”. Amesisitiza Waziri Bashe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad