HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 20, 2021

MKOA WA RUVUMA WASHIKA NAFASI NZURI KITAIFA UKUSANYAJI WA MAPATO

 


MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Chritina Mndeme amewapongeza Wakurugenzi watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kusimamia ukusanyaji wa Mapato kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambapo Halmashauri zote nane zimevuka  asilimia 80 na kufanya Mkoa kuwa katika nafasi nzuri Kitaifa.

Mndeme pia ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Mkoa wa Ruvuma kwa kufanya kazi nzuri ya kukusanya Mapato ya ndani  ya Mkoa  katika kipindi cha mwaka 2019/2020 na kuweza kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 15 sawa na asilimia 94.

“Naipongeza Halmashauri ya Tunduru  kwa kukusanya Mapato ya Ndani kwa asilimia 121.87,pia naipongeza Halamashauri ya Manispaa ya Songea tangu  imeanza kutumia stendi kuu ya Shule ya Tanga Januari1,2021  imeongeza mapato kutoka shilingi 200,000 mpaka  970,000 kwa  siku”,alisema.

Mndeme amesema Mkoa unatarajia kuimarika kiuchumi kwa kuongezeka kwa mapato yatokanayo na kodi pamoja na ushuru kwasababu Barabara ya Ushoroba wa  Mtwara imefunguka na kupelekea kutoa fursa nyingi za kibiashara na kiuchumi.

Hata hivyo amesema biashara ambazo zinapatikana maeneo mengine Nchi Jirani za Malawi na Msumbiji yanaunganishwa kwa kupitia usafiri wa Ndege kupitia Uwanja wa ndege wa Songea na barabara ya lami ya Mtwara corridor.

Amesema Meli katika Ziwa Nyasa zimeanza kazi za Usafirishaji baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Meli ya abiria ya MV Mbeya  II Januari 5,2021 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Kassim Majaliwa ambayo inabeba abiria  300 na Mizigo tani 200.

Hata hivyo Mndeme amewaagiza Wakurugenzi kusimamia Mapato yatokanayo na Kodi pamoja na Ushuru amesema fedha hizo hutumika katika kujenga miradi ya maendeleo ikiwemo vituo vya Afya,Barabara,Ununuzi wa Ndege,Ujenzi wa Reli na  huduma nyingine za kijamii.

Ameziagiza Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma kubuni na kupanua wigo wa mapato kwa kuhimiza watu kudai Risiti na wafanyabiashara  kutoa risiti kila wanapouza  bidhaa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad