MAKANDARASI NCHINI WATAKIWA KUSOMA MIKATABA YAO KWA MAKINI KABLA YA KUISAINI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 30, 2021

MAKANDARASI NCHINI WATAKIWA KUSOMA MIKATABA YAO KWA MAKINI KABLA YA KUISAINI

 

 MAKANDARASI nchini wametakiwa kuwa wanasoma mikataba yao kwa makini kabla ya kuisaini ili waweze kutambua wajibu wao wakati wa utekelezaji wa mkataba husika.

Pia wameaswa kuwa wanaurudia mkataba wao mara kwa mara pindi wakiwa  wanaufanya kazi ili kujua kama bado kwenye njia sahihi ama wa wanatoka nje ya mkataba.

Msajilil wa Bodi ya Wakandarasi, Rhoben Nkori ameyasema hayo leo Januari 29, 2021 wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa makandarasi kujifunza namna ya kusimamia mikataba, bima na matumizi ya mtandao (Taneps) yaliyoandaliwa na Bodi ya Wakandarasi (CRB) nchini

"Mafunzo haya ni muhimu sana kwa makandarasi kwa sababu suala la usimamizi wa mikataba ni muhimu sana na ndio unaamua utekelezaji mzima wa mkataba kwani ukishindwa kutumia mkataba maana yake unashindwa kujua haki zako na wajibu wako katika kufanya kazi" amesema Nkori.

"Kuna suala la kusaini, pia kuna suala la kusoma mikataba ukaijua, ukajua wajibu wako ni nini katika mkataba huo na kujua haki zako ni nini na kama zimeainishwa vizuri kwenye mkataba na baada ya kuelewa unaingia mkataba ukishasaini unautekeleza kwa kufuata mkataba" ameongeza.

Kwa upande wake mkandarasi Idrisa Kinyagu kutoka kampuni ya ukandarasi ya Powers and Network Backup Ltd ya jijini Dar es Salaam amesema, mafunzo hayo yamekuwa msaada mkubwa kwao makandarasi

Tumejifunza namna ya kusimamia mikataba yetu, bima na jinsi ya kutumia mfumo wa kuwasilisha zabuni kupitia mtandaoni.

Mifumo hiyo mitatu ambayo CRB wametufundisha imetupa mafanikio makubwa sana, kwa sababu kuna sehemu tulikuwa na matatizo ya namna ya kusimamia mikataba yetu na wateja, Lakini kupitia mafunzo haya, tumepata maarifa ambayo yatatusaidia kuhakikisha namna ya kufanikisha kazi kwa ufanisi kati ya mkandarasi yoyote na mteja pindi mnapoingia mkataba.
 
Vilevile katika suala la matumizi ya bima na mtandao tumejifunza vingi, saizi mtu unaweza ukapata zabuni mtandaoni na kumalizana nayo moja kwa moja bila ya
kulazimika kwenda mwenyewe kuipeleka na kupoteza muda.

Naye, Philomena Malenda, mkandarasi kutoka kampuni ya wakandarasi ya Progressive Women ameishukuru CRB kwa kuwapatia mafunzo hayo, na sasa wanajua nini cha kufanya pindi wakiingia mkataba hata kama wakikutana na changamoto mbali mbali.

"Kwa kweli, Taneps imetusaidia kwa kiasi kikubwa sana ukilinganisha na zamani ambapo sasa inatusadia matumizi ya muda na kuepuka mlolongo mrefu wa kufikisha zabuni yako kwa kuwa ukitumia mtandao kazi yako inafanyika mahali popote pale,  ameongeza kuwa serikali inawasaidia sana.

Msajili wa Bodi ya Wakandarasi nchini, Rhoben Nkori akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufunga mafunzo ya siku tatu kwa yalioandaliwa na Bodi ya Wakandarasi (CRB) kwa makandarasi kutoka sehemu mbali mbali nchini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Bodi ya Wakandarasi nchiji, Rhoben Nkori akizungumza na makandarasi wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa makandarasi ya kuwapa maarifa namna ya kusimamia mikataba yao, matumizi ya bima na kutumia mitandao kupata Zabuni. yaliyofanyika jjjini Dar es Salaam
Mkandarasi kutoka kampuni ya wakandarasi ya Progressive Women, Philomena Malenda akizungunza na waandishi wa habari kuelezea namna atakavyoyatumia mafunzo waliyopatiwa na CRB katika kufanikisha kazi zao hususani mikataba watakayoingia
Idrisa Kinyagu kutoka kampuni ya wakandarasi ya Power and Network Backup ltd ya jijini Dar es Salaam, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza mafunzo ya siku tatu yaliyoandaliwa na CRB jijini Dar es Salaam.
 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad