HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 30, 2021

DKT. KIJAZI AWATAKA WATUMISHI KUWA NA RATIBA YA MICHEZO

 




 

Na Happiness Shayo – Dodoma

NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi amewataka watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao na kujenga mshikamano na upendo katika maeneo yao ya kazi.

Dkt. Kijazi ametoa wito huo wakati wa bonanza la watumishi lililoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii lililofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

''Mazoezi iwe ni sehemu ya maisha yetu na pia iwe ni sehemu ya kazi zetu² amesisitiza Dkt. Kijazi.

Ameongeza kuwa, Wizara yake itajipanga kuhakikisha kila mtumishi anashiriki katika kufanya mazoezi na pia kila mtumishi anashiriki kwenye mabonanza na amewataka watumishi kuendelea kuhamasishana ili ushiriki uzidi kuongezeka katika matamasha yanayokuja.

Dkt. Kijazi amefafanua kuwa Wizara itaweka utaratibu wa kuwatambua washiriki bora wa kila mwaka wanaofanya mazoezi na wanaoshiriki kikamilifu katika matamasha kama hayo na kuwapa zawadi maalumu.

Pia, amesema kuwa, Wizara itahakikisha ushiriki wa watumishi katika matamasha hayo hauishii Dodoma bali utaendelea kwenye matamasha mengine yanayofanyika nchini, kama Kilimanjaro Marathon, Ngorongoro Marathon na Serengeti Marathon.

'' Watumishi watakaofanya vizuri tutawadhamini ili waiwakilishe Wizara kwenye Marathon hizo.''Amesema.

Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Kijazi amewapongeza washiriki wote walioweza kukimbia mbio za kilomita tano kwa kupata medali na kuwataka ambao wameshindwa wajitahidi kipindi kijacho wamalize mbio hizo.

''Ni imani yangu kuwa bonanza linalokuja wote tutamaliza mbio za kilomita tano, cha msingi tuendelee kufanya mazoezi ,tusisubiri hadi matamasha haya yafike ndo tufanye mazoezi.'' Dkt. Kijazi amesema.

Dkt. Kijazi amewashukuru Dodoma Fitness Club na Muungano Fitness Club kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kufanikisha bonanza hilo  na kusema kuwa uwepo wao ni chachu kwa Wizara katika  kuimarisha mabonanza.

Naye, Mwenyekiti wa Jogging Clubs Dodoma, Bw.Mugisha Mujungu ameahidi kuendelea kushirikiana na Wizara kila itakapohitaji ushirikiano katika kufanya mazoezi na kuwataka watumishi wa serikali kujiunga na Jogging Clubs ili kuimarisha afya zao.

Bonanza hilo limehudhuriwa na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na washiriki kutoka Dodoma Fitness Club na Muungano Fitness Club za Dodoma.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad